Katibu Mkuu mpya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji), Bi. Dorothy Mwaluko akikabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Profesa, Faustin Kamuzora ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Tawala mkoani Kagera. Kabla ya uteuzi huo Bi. Mwaluko alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejineti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, leo, tarehe 16 Januari, 2018.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Bi. Maimuna Tarishi akishuhudia makabidhiano rasmi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Katibu Mkuu mpya (Sera na Uwekezaji), Bi. Dorothy Mwaluko kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Profesa, Faustin Kamuzora ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Tawala mkoani Kagera. Katibu Mkuu Mwaluko kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejineti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, leo, tarehe 16 Januari, 2018.
 Aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora akishukuru kwa ushirikiano aliokuwa anapewa wakati akihudumu katika ofisi hiyo, kwa Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Bi. Maimuna Tarishi (katikati) na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko (kushoto ), Ofisi ya na, leo, tarehe 16 Januari, 2018.
 Aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora akiwa katika picha ya pamoja na waliokuwa Makatibu Muhtasi wake, pamoja na Katibu Mkuu mpya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko (kulia), mara baada ya Profesa Kamuzora kumkabidhi ofisi rasmi, leo, tarehe 16 Januari, 2018.
Katibu Mkuu mpya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji), Bi. Dorothy Mwaluko ambaye ameteuliwa hivi karibuni. Kabla ya uteuzi huo Bi. Mwaluko alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejineti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, leo, tarehe 16 Januari, 2018. (PICHA ZOTE NA ; OFISI YA WAZIRI MKUU).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: