Mwenyektiti w Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, ,Maliasili na Utalii, Nape Nnauye akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo akiwaonesha kundi la tembo mara baada ya kamati hiyo kufanya utalii nyakati za jioni mwishoni mwa wiki wakati Kamati hiyo ilipomaliza kufanya kikao cha kujadili mradi wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini katika Hifadhi ya taifa ya Ruaha koani Iringa. (Picha na Lusungu Helela-MNRT)
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Constantine Kanyasu (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja kwenye jabali ambalo watalii hupanda katika jiwe hilo kwa ajili ya kuona makundi ya wanyama aina ya kiboko wakiwa wanakunywa maji katika mto wa Ruaha Mkuu katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa mwisho ni wa wiki wakati kamati hiyo ilipofanya utalii wakati Kamati hiyo ilipomaliza kikao cha kujadili mradi wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini . (Picha na Lusungu Helela-MNRT)
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maliasili na Utalii, Neema Mgaya akiwa ameongoza na Mwenyekiti wa Kamati nhiyo, Nape Nnajuye pamoja na wajumbe wengine wakitelemka katika eneo la kuonea wanyama aina ya viboko nyakati za jioni wanapokunywa maji mto wa Ruaha Mkuu katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa mwisho ni wa wiki wakati kamati hiyo ilipofanya utalii wakati Kamati hiyo ilipomaliza kikao cha kujadili mradi wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini . (Picha na Lusungu Helela-MNRT).
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Maliasili na Utalii, Mwita Getere akiwa ameongozana na wajumbe wengine wakipanda ngazi juu ya sehemu ya kuonea wanyama aina ya viboko nyakati za jioni wanapokunywa maji mto wa Ruaha Mkuu katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa mwisho ni wa wiki wakati kamati hiyo ilipofanya utalii wakati Kamati hiyo ilipomaliza kikao cha kujadili mradi wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini . (Picha na Lusungu Helela-MNRT).

NA LUSUNGU HELELA-IRINGA.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu amewataka Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa chachu ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa wananchi wanawaongoza kwa kutenga muda wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Imeelezwa kuwa hamasa ya wananchi ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini imekuwa na mwitikio mdogo ukilinganisha na idadi ya watalii wa kutoka nje.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara ya siku mbili ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kukuza na kuendeleza utalii Kusini katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa.

Amesema endapo kila Mbunge kwa nafasi yake ataweza kuhamasisha wananchi kutembelea vivutio vya utalii mapato yataweza kuongeza maradufu kupitia Utalii wa ndani tofauti na ilivyo sasa.

"Tengeni muda wa kupumzika baada ya pilikapilika ya kuwahudumia wapiga kura wenu, unakuja huku Ruaha unapumzisha akili huku ukijipanga mwaka 2020 kwa ajili ya uchaguzi Mkuu" alisema.

" Tusisubiri tuje kikazi kama tulivyokuja hivi, Panga njoo na familia yako ufurahie maisha mara moja moja sio mbaya" Alisisitiza Kanyasu.

Pia, Kanyasu aliwaomba Wabunge hao kila wanapopata nafasi ya kukutana na wananchi majimboni mwao wawahamasishe kutembelea vivutio vya utalii ili kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa jitihada anazofanya za kutaka kuongeza mapato yatokanayo na sekta ya utalii.

Amesema ufufuaji wa kampuni la usafiri wa ndege nchini (ATCL) kwa kununua ndege saba achilia mbali mradi wa reli ya Standard Garge ni juhudi wazi za Rais John Magufuli kuona sekta ya utalii inagusa maisha ya kila wananchi kimapato.

Katika hatua nyingine, Kanyasu aliwaomba Wabunge hao wawahamasishe wananchi kuchangamkia fursa za utalii kwa kujenga Hoteli au kwa kuanzishavituo vya utalii wa kiutamaduni ambao umekuwa ukipendwa sana na watalii wengi wa kutoka nje.

Aidha, Mhe.Kanyasu aliwaeleza Wabunge hao kuwa baada ya kufungua utalii Kusini, Serikali inakusudia kufungua utalii katika kanda nyingine ikiwemo ya kanda ya ziwa na kanda ya Kaskazini Magharibi, Hivyo wawaandae wananchi wao kuchangamkia fursa za utalii badala ya kubaki walalamikaji.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mtama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Nape Nnauye alisema kufunguliwa mapema kwa utalii Kusini kutatoa picha halisi kwa wananchi katika kunufaika kiuchumi kupitia sekta hiyo katika kanda nyingine

Pia, Mhe, Nape aliishauri Serikali kulifanyia kazi suala la tozo ya kuingia ndani ya hifadhi (single entry) kutokana na malalamiko ya muda mrefu wanayoyatoa wananchi kwanaoishi Katibu na Hifadhi kuwa imekuwa ikiwabana watalii kutoka nje ya Hifadhi kuwatembelea wananchi hao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: