Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Sekta ya Ulinzi Tanzania (TSIA), ambapo aliwaasa viongozi wa kampuni hizo kuwadhibiti walinzi wao kutojihusisha na masuala ya uhalifu.Ufunguzi huo umefanyika leo, jijini Dodoma.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Narcis Misama akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Sekta ya Ulinzi Tanzania (TSIA), ambapo aliwahakikishia wanachama wa chama hicho ushirikiano kutoka Jeshi la Polisi. Ufunguzi huo umefanyika leo, jijini Dodoma.
Mdau wa Masuala ya Ulinzi, ambae pia ni Inspekta Jenerali Mstaafu, Said Mwema akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Sekta ya Ulinzi Tanzania (TSIA).Ufunguzi huo umefanyika leo, jijini Dodoma.
Wanachama mbalimbali wa Chama cha Sekta ya Ulinzi Tanzania (TSIA), wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa Mkutano Mkuu wa chama hich, uliofanyika leo, jijini Dodoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Serikali imeziasa Kampuni Binafsi za Ulinzi kutoshiriki katika matukio ya uhalifu baada ya kuripotiwa mara kwa mara kwa walinzi wa kampuni hizo kupatikana na hatia ya uhalifu katika mahala pao pa kazi ikiwemo kuwaazima silaha wahalifu kwenda kufanya matukio ya uhalifu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Sekta ya Ulinzi Tanzania (TSIA), uliofanyika leo jijini Dodoma.

Amesema kampuni zinatakiwa kuongea na walinzi wao sambamba na kuongeza maslahi kwa walinzi hao ili wasiingie katika vishawishi hali itakayopelekea kutoshiriki katika matukio ya uhalifu sehemu zao za kazi.

“Baadhi ya walinzi wa kampuni mnazozisimamia wamekua wakishiriki katika uhalifu, wengine wameenda mbali zaidi kwa kuwaazima silaha wahalifu kwenda kufanyia uhalifu, jambo hili halikubaliki, sasa naziagiza kampuni zenye walinzi wa namna hii kuhakikisha vitendo hivi vinakoma mara moja,” alisema Masauni.

Akizungumza kwa niaba ya Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Narcis Misama alisema wao kama jeshi wanawahakikishia wanachama hao wa sekta ya ulinzi ushirikiano utakaowasaidia kutimiza majukumu yao huku akiweka wazi jeshi kama jeshi haliwezi kuyafikia maeneo yote kwa wakati.

“Nawashukuru sana kwani mmekua msaada muhimu kwa jeshi la polisi hasa pale uhalifu unapotokea maeneo mnayolinda, tumeweza kuwapata watuhumiwa wa matukio mbalimbali kupitia taarifa zenu pindi tu uhalifu unapotokea, nawaahidi ushirikiano kwa siku zijazo zaidi ya mnaoupata kutoka kwa jeshi,” alisema SACP Misama

Akizungumza kwa niaba ya wanachama Mwenyekiti wa Chama cha Sekta ya Ulinzi Tanzania, Felix Kagisa aliiomba serikali ipitishe sharia zinazoongoza sekta ya ulinzi binafsi ili waweze kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: