Mkurugenzi wa Tamasha la Busara, Yusuf Mahmoud akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam kuelezea jinsi walivyoweza kujipanga kuwapa burudani wakazi wa Zanzibar kuanzia Feb 7-10 ndani mji mkongwe. Pembeni yake ni Balozi wa Norway nchini Tanzania, Bi. Elisabeth Jacobsen (katikati) na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Tamasha la Sauti za Busara Bi. Julia Bishop (kwanza kulia). Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Bi. Elisabeth Jacobsen akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo kuelezea machache jinsi walivyoweza kujipanga kuthamini tamasha la Sauti za Busara linalotarajia kufanyika Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Tamasha la Sauti za Busara Bi. Julia Bishop (wa tatu toka kulia) akizungumzia jinsi ambavyo Tamasha hilo limekuwa msaada mkubwa katika kutangaza utamaduni wa mwafrika. Wengine ni Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud (kwanza kushoto), Balozi wa Norway nchini Tanzania, Bi. Elisabeth Jacobsen na Meneja wa Tamasha la Sauti za Busara Journey Ramadhani.
Wageni waalikwa wakiwa katika mkutano wa wanahabari.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Tamasha la 16 la Sauti za Busara linatarajia kuanza Zanzibar mwezi febuari 7 hadi 10 kwa miondoko ya kiafrika huku kauli mbiu yake ikisema 'POTEZEA RUSHWA SIYO DILI'.

Tamasha la Sauti za Busara limeungana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupinga matumizi ya Rushwa katika jamii.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mahmoud amesema kuna kila sababu ya kusherehekea tukio hilo msimu huo, kutokana na wasanii waliochaguliwa na bei za tiketi.

"Zanzibar itawakaribisha wapenzi wa muziki kutoka katika Kila Kona ya dunia,wakijumuika pamoja kusherehekea upekee wa Sauti kutoka nchi ya Algeria hadi Zimbabwe kutoka Cape Town hadi Casablanca " alisema Mahmoud.

Hata hivyo Mahmoud ameeleza lengo la tamasha hilo ni kuwatangaza wasanii wachanga na wale wanaochipukia kutoka Afrika Mashariki.

Pia ametaja bendi kama wamwiduka kutoka Mbeya na Skide kijana anayefanya muziki wa aina ya singeli ambao asili yake halisi ni Tanzania na kwa sasa unakaribia kuuteka ulimwengu.

Aidha ametaja lengo la kuwepo tamasha la Sauti za Busara si tu kwa ajili ya kuburudisha watu bali pia kuelimisha jamii na kuangaza maovu yanayoletwa na rushwa likiwa kama tatizo linaloendelea kuwanyima vijana haki zao za kimsingi na hasa wanamuziki wa kike.

Kwa upande wake Meneja Journey Ramadhan amesema kuwa tamasha la Sauti za Busara linatangaza Tanzania na Zanzibar na ulimwengu kote kupitia muziki.

Ramadhan ameeleza jinsi gani tamasha hilo linawavuta karibu waandaji wa matamasha wa kimataifa ,linawapa fursa wanamuziki wetu kuwasilisha kazi zao kwa hadhira ya kimataifa

"Orodha ya mwaka huu inayo wasanii kama Fid Q , Damian soul,Mkubwa na wanawe crew ,stone Town rockerz, Tausi women's Taarab ,Rajab Suleiman,Kithara,Afrigo band , Jackie Akello na Eli Maliki (Uganda) Fadhilee itulya na shamsi Music kutoka Kenya." alisema Ramadhan

Hata hivyo tamasha la sauti za busara linadhaminiwa na ubalozi wa Norway , ubalozi wa uswis nchini Tanzania na Zambia, Umoja wa Ulaya, Africalia, Ubalozi wa Ujerumani na Shirika la Ethiopia na Zanzibar Media Corporation.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: