Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akizungumza wakati akifungua warsha ya wahariri kuhusu bajeti yenye mrengo wa kijinsia katika ukumbi wa ofisi za TGNP Mtandao jijini Dar es salaam. Picha zote na Kadama Malunde - na Frankius Cleophace Malunde1 blog.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akielezea kuhusu dhana nzima ua bajeti yenye mrengo wa kijinsia.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.
Regina Mziwanda wa BBC Swahili akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
Warsha inaendelea...
Mhariri wa gazeti la Majira,Imma Mbuguni akichangia hoja ukumbini.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.

TGNP Mtandao imeendesha warsha kwa Wahariri na baadhi ya waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchini kuhusu bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa ajili ya kuwaongezea uelewa na uwezo kuhariri na kuripoti masuala ya kijinsia.

Warsha hiyo ya siku moja imefanyika Jumamosi Januari 19, 2019 katika ofisi za TGNP Mtandao zilizopo jijini Dar es salaam.

Akifungua warsha,Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi alisema mafunzo hayo yawawezesha wahariri na waandishi wa habari kuhamasisha uingizwaji wa masuala ya kijinsia katika mipango,miongozo na sera za serikali.

"Tumekutana hapa kwa ajili ya kukumbushana dhana kuu za jinsia na umuhimu wa kuzingatia masuala ya jinsia kwa maendeleo lakini pia kuweka mikakati ya namna ya kuongeza kasi ya kuripoti masuala ya kijinsia katika vyombo vya habari kwani tunaamini vyombo vya habari ni muhimu kwa maendeleo ya jamii",alisema Liundi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: