Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akifanya mahojiano kwenye kipindi cha "Jambo Tanzania" kinachoruka TBC 1 akielezea mikakati ya wizara hiyo jinzi ilivyojipanga kutangaza vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi kupitia Bodi ya Taifa ya Utalii leo Mikocheni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mtangazaji wa TBC1, Mbozi Katala
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akifanya mahojiano kwenye kipindi cha "Asubuhi Hii " kinachoruka TBC TAIFA akielezea mikakati ya wizara hiyo jinzi ilivyojipanga kutangaza vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi kupitia Bodi ya Taifa ya Utalii leo Mikocheni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mtangazaji wa TBC TAIFA, Asha Haji. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA).

Na Lusungu Helela -USUNGU HELELA-DSM.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema Serikali inaangalia namna bora ya kuiwezesha Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo badala ya kila Taasisi kujikuta ikitangaza vivutio vya Utalii ilivyonavyo kivyake .

Ameyasema hayo leo Jumatano Januari 9, 2019 wakati alipokuwa akifanya mahojiano kwenye kipindi cha "Jambo Tanzania" kinachoruka TBC1na kipindi cha "Asubuhi Hii" kinachoruka TBC Taifa Mikocheni jijini Dar es Salaam

Aidha, ameitaka TTB ianze kutangaza vivutio vya utalii kwa mfumo wa vifurushi (Packages) ili watalii wanapokuja waweze kutembelea sehemu mbalimbali za vivutio badala ya kwenda moja kwa moja Hifadhi ya Taifa ya Serengeti au Ngorongoro pekee.

" Tunataka mtalii kabla hajafika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha aende akaone jiwe la maajabu la Gangilonga akitoka hapo apitie Boma la Mjerumani ndo aende zake Ruaha" amesema Mhe.Kanyasu.

Pia amesema Wizara inajipanga kuanza kutumia watu maarufu wakiwemo wasanii pamoja na wacheza mpira kwa kuwadhamini lengo likiwa ni kutangaza vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: