Mfanyabiashara matunda akiwahudumia wateja wake huku akiwa amevaa kitambulisho cha wajasiriamali kama alivyokutwa leo katika kituo cha mabasi Makumbusho jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka, (MMG).
Mfanyabiashara wa vitu mbalimbali akiwahudumia wateja wake huku akiwa amevaa kitambulisho cha wajasiriamali kama alivyokutwa leo katika kituo cha mabasi Makumbusho jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka, (MMG).

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

WAFANYABIASHARA wadogo katika soko la Tandika wamemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwapatia vitambulisho ambavyo vinawasaidia katika kufanya kazi zao kwa uhuru sasa.

Wakizungumza na blogu ya jamii wafanyabiashara hao wameeleza kuwa kabla ya kupatiwa vitambulisho hivyo walikuwa wanakumbana na changamoto ya kupigwa na kuchukuliwa bidhaa zao na mgambo wa jiji ila kwa sasa wanafanya biashara hiyo kwa uhuru kabisa.

Aidha wameutaka uongozi wa soko hilo kuwa karibu nao ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili na kuzipatia utatuzi.

Pia wamewataka wafanyabiashara wengine kujitokeza ili waweze kupatiwa vitambulisho hivyo ambavyo vitawasaidia katika kufanya shughuli mbalimbali zitakazowasaidia kujikwamua kiuchumi.

Wamemtakia afya na heri Rais Magufuli katika kazi zake zinazogusa wananchi wengi hasa wa hali ya chini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: