Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akishuhudia utokaji wa maji eneo la  Kata ya Wazo mara baada ya kukamilika kwa tanki kubwa litakalowapatia maji kwa kipindi cha mwaka mzima bila kukatika.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akiongea na wananchi waliojitokeza kuchota maji.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akiongea na wananchi waliojitokeza kuchota maji huku akitoa maelekezo ya kuuza maji kwa tsh. 50 kwa ndoo tu.

Maji yakitoka.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akipata maelezo toka kwa  Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) imeanza kuwasambazia maji wananchi wa Kata ya Wazo na vitongoji vyake ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotoa jumapili Jan 13, 2019.

DAWASA imewekeza na imejenga tanki kubwa lenye uwezo wa kihifadhi lita milioni sita itakayofanya wakazi wa kupata maji kwa kipindi chote bila mgao.

Akizungumza na wananchi mara baada ya kumaliza kazi na kuwapatia wananchi maji, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa amewaomba wasimamizi wa vizimba (Maduka ya kuuzia maji) kuuza maji kwa tsh. 50 kwa ndoo na si tsh. 100 kama ilivyokuwa awali.

"Leo mnafurahi kufunguliwa maji ila naomba muuze maji tsh. 50 kwa ndoo, sitaki kuona wananchi wanalalamika eti bei kubwa, mimi ndiyo msimamizi naomba mtekeleze mkumbuke na kulipa ankara zenu za maji ili DAWASA waweze kuwahudumia vyema," amesema.

Mwishoni kwa wiki iliyopita DAWASA kupitia Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja mbele ya wananchi akiwemo Mkuu wa Wilaya Kinondoni Daniel Chongolo, aliwaahidi wakazi wa kata ya Wazo na vitongoji vyake kuanzia wiki hii maji watapata bila mgawo wowote.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: