Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Mhandisi Aron Joseph akifunga warsha kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Miradi ya MajiTaka kwa wageni waliofika katika warsha ya siku moja ya kujengeana uwezo baina ya TANZANIA NA KENYA juu ya mafanikio na changamoto zinazowakabili. Wageni hao ni maofisa wa Serikali ya Kenya kutoka Kampuni ya Majisafi na Majitaka Nairobi (NCWSC) na Huduma za jamii, Mashirika binafsi na viongozi wa vikundi vya jamii ambao walikuja nchini Tanzania kwa siku 5 wakitembelea Dar es Salaam na Mwanza. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI) Tim Ndezi akiwatambulisha wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Miradi ya MajiTaka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) katika warsha ya siku moja ya kujengeana uwezo baina ya TANZANIA NA KENYA juu ya mafanikio na changamoto zinazowakabili.
Wageni na wenyeji wakifuatilia mkutano huo.
Mhandisi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI), Festo Dominick Makoba ambaye ndiye msimamizi wa eneo la Vingunguti jijini Dar es Salaam katika mradi wa vyoo vya kisasa kwa wananchi.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha DAWASA, Neli Msuya akiwashuru wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) mara baada ya kumaliza mkutano.


Mmoja ya maofisa wa Serikali ya Kenya waliofika Tanzania Bw. Patrick Njoroge wa Akiba Mashirani Trust akielezea hali halisi ya jimbo jipya la Mukuru, Nairobi- Kenya ambalo mipango mji wake haujapangika.
 Bi. Kellen Muchira kutoka Shirika la Caritas Switzerland akizungumza machache.
Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Mhandisi Charles Makoye akiwaelezea juu ya miradi wa kuchakata MajiTaka inayosimamiwa na kuendeshwa na DAWASA kwa wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI.
Mmoja ya wageni kutoka nchini Kenya Nancy akitia shukrani zake za peke kwa DAWASA na CCI kwa kuweza kuwapokea na kuwatembeza kujionea miradi mbali mbali ya MajiTaka jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mji Mpya, Kata ya Vingunguti Rahimu Seif Gassi akitoa shukrani kwa wageni kutoka nchini Kenya waliofika Tanzania kwa ajili ya kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu Maji Taka kupitia Shirika la CCI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) mara baada ya kumaliza mkutano.
Picha ya pamoja.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

WAKENYA wamefurahishwa na jinsi Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka ilivyojipanga katika kusaidia wananchi ili kuwaondolea kero ya MajiTaka kupitia miradi yake.

Miradi ya MajiTaka iliyowavutia ni ule wa Kigamboni na Vingunguti jijini Dar es Salaam ya kuwa jengea vyoo wananchi ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu juu ya kusimamia kutipia wadau wao Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Kijamii nchini (CCI Tanzania).

Akizungumza mmoja ya maofisa wa Serikali ya Kenya waliofika Tanzania Bw. Patrick Njoroge wa Akiba Mashirani Trust amesema binafsi amefurahishwa kwanza na ujio wao umekuja kujifunza masuala ya MajiTaka kwa vile nchini Naironi kuna eneo la Mukuru limetangazwa kuwa jimbo jipya hivyo wao wamepewa kazi ya kupanga mfumo mzima wa majisafi na Majitaka.

 "Binafsi niwavutiwa sana na jinsi DAWASA mlivyoweza kuzuia milipuko ya magonjwa kwa kuwawekea wananchi wenu mifumo mizuri ya majitaka kwa kuwajengea vyoo kupitia wadau wenu CCI, hatuna budi tukirudi kule tutatoa mapendekezo mazuri na ikiwezekana mradi huu utaanza na kwetu," amesem Njoroge.

Njoroge ameongeza kuwa jimbo jipya la Mukuru lililopo Nairobi linafanana kabisa na Mazingira mabovu yasipo rasmi kama ya Vingunguti, na wananchi wake wengine wanaishi katika vijumba vya mabati na wengine wamechukua mantanki makubwa na kufanya nyumba hivyo teknolojia waliyotumia CCI Tanzania itafaa hata huko kwao.

Upande wake Bi. Kellen Muchira kutoka Shirika la Caritas Switzerland lililpo Kenya amesema kazi waliyopewa na serikali yao ya Kenya inafikia mwisho kwa kupitia maeneo yote ambayo wanao kwao itakuwa ni rasmi kusoma mazingira na kwenda kutoa mrejesho ili mambo yasonge mbele.

"Kazi yetu tuliyopewa imefika mwisho hivyo hatuna budi kwenda kutoa mapendekezo yatakayoweza kufanya jimbo la Mukuru kuwa la mfano kwa kuweza kuwepa mipango iliyobora kuwasaidia wananchi.

Awali akifungua warsha hiyo Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA,  Mhandisi Aron Joseph ambaye akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu amewakaribisha wageni na kuwaambia wamefikia mikono salama na kuwa DAWASA imejipanga zaidi kuwatatulia wananchi matatizo ya Majisafi na Majitaka kwa kumaliza miradi ya majisafi ya Kimbiji na Mpela na miradi yote ikiwemo lile tanki la Kibamba na Kisarawe.

Upande wa MajiTaka amesema kwa sasa wanayo miradi mbali mbali ikiwemo huo wa kuwajengea vyoo salama wakazi wa Vingunguti kupitia CCI, Toangoma ambao wakazi wa Kigamboni hawapati shida sehemu ya kupeleka majitaka kwa vile unaweza kupokea lita 10,000 kwa siku huku akiongezea miradi ya Mlalakuwa, Mburahati na Temeke Wires.

"Tumejipanga kutoa huduma bora kwa wananchi wa Dar es Salaam na Pwani kwa kiwango cha juu kabisa, tunangoja kufungua milango mwezi ujao kwa kuweza kupata fedha zaidi ili kuendeleza miradi mingi zaidi, niwaombe mkienda huko kwenu mje tena muone tulivyosomba mbele," amesema Mhandisi Aron Joseph.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: