Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Zanzibar Felix Wandwe (suti nyeusi), Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Muhambwe Dk. Gabriel Chitupila na baadhi ya Maafisa wa NEC wakiangalia orodha ya majina ya Wapiga Kura iliyobandikwa nje ya Kituo cha Kupigia Kura kilichojengwa katika eneo la wazi la uwanja wa Mpira wa Magereza katika Kata ya Biturana wilayani Kibondo. Kata hiyo inafanya uchaguzi mdogo wa Udiwani Januari 19, 2019.
 Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo Dk. Gabriel Chitupila akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Zanzibar Felix Wandwe (suti nyeusi) kuhusu maandalizi ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Biturana mara baada ya kutembelea Kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Nengo wilayani humo.
 Baadhi ya wakazi wa Kata ya Biturana katika Halmashauri ya wilaya ya Kibondo wakikagua majina yao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililowekwa wazi katika eneo lao. Uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata ya Biturana utafanyika Januari 19 mwaka huu ukihusisha vyama 3 vya Siasa.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Zanzibar Felix Wandwe (suti nyeusi), Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo Dk. Gabriel Chitupila na baadhi ya Maafisa wa NEC wakikagua vituo vya kupigia Kura katika Kata ya Biturana wilayani humo itakayofanya uchaguzi mdogo wa Udiwani Januari 19, 2019.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Zanzibar Felix Wandwe akizungumza na wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi (hawapo pichani) watakaosimamia uchaguzi mdogo wa udiwani Katika Kata ya Biturana wilayani Kibondo Januari 19 mwaka huu. Picha na NEC – Kibondo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: