Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Mradi wa Kimbiji na Mpera Mhandisi Shiyenze (wa nne toka nne) Bunyese mara baada ya kutembelea katika kisima cha K-17, K-11 na K-3 ambavyo vipo katika hatua ya mwisho ili wananchi waweze kupatiwa maji safi na salama.
Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo mafupi toka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mamlaka ya Maji safi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Lydia Ndibalema (wa pili toka kushoto) juu ya mradi wa visima vya Kimbiji na Mpera uliopo Kimbiji, Kigamboni jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa wasimamizi pamoja na mkandarasi wanaosimamia miradi ya Mradi wa Kimbiji katika kisima cha K-17, K-11 na K-3 ambavyo vipo katika hatua ya mwisho ili wananchi waweze kupatiwa maji safi na salama.
Waziri wa Maji na Umwagiliziaji Pro. Makame Mbarawa akizungumza na wanahabari mara baada ya kumalizia ziara yake ya kutembelea mradi wa Kimbiji na Mpera katika kisima cha K-17, K-11 na K-3 ambavyo vipo katika hatua ya mwisho ili wananchi waweze kupatiwa maji safi na salama. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amewataka wataalamu wanaokabidhiwa majukumu kufanya kazi, wakamilishe miradi kwa wakati ili kuwapatia wananchi huduma.

Ameyasema hayo wakati alipotembelea mradi wa Visima 20 vya Kimbiji na Mpera vyenye jumla ya thamani ya Bilioni 23.

Akizungumza baada ya ziara hiyo, Prof Mbarawa amesema kuwa visima 12 vya Kimbiji tayari vimeshakamilika katika uchimbaji kilichobaki ni kupima wingi wa maji na ubora wake (Pump test).

Mbarawa amesema, kwenye visima hivyo viwili vipo tayari kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kwa wananchi ili wapate maji safi na salama.

“ Kulikua na changamoto kidogo ya mkandarasi ila kwa sasa kila kitu kipo sawa, anayesubiriwa ni Mshauri (Consultant) kwa ajili ya kuja kushauri kuhusu upimaji wa wingi wa maji na ubora ili tuendelee na mchakato wa huduma ya maji kwa wananchi,” amesema Mbarawa.

“Visima nane kati ya 20 vilivyopo Mpera vipo katika hatua ya Kati ya uchimbaji na nawashauri DAWASA kumaliza kwanza visima vya Kimbiji ili baadae wahamie hivyo vya Mpera, “amesema

Mbarawa ameutaka uongozi wa DAWASA kuharakisha katika manunuzi na kumpata Mkandarasi ili kufikia mwishoni mwa Mei mwaka huu wananchi wa Kimbiji na Kigamboni waweze kupata maji.

Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mamlaka ya Maji safi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Lidya Ndibalema amesema mradi huu ulikuwa na thamani ya Bilioni 23 mpaka sasa wameshatumia bilioni 17 n kikubwa kwa visima vya Kimbiji ni Mshauri (Consultant) ni kuja kutoa maelekezo katika Pump Test.

Ndibalema amesema tayari ujenzi wa tanki la Kibada upo katika hatua ya manunuzi na wamefuata maelekezo kama tuliyoagizwa na serikali na ikishakamilika tutaanza mchakato wa kuanza ujenzi.

Mradi wa Kimbiji na Mpera unazalisha maji takribani milioni 250 kwa siku ikiwa ni nusu ya maji yanayozalishwa kwa Mkoa mzima wa Dar es Salaam Lita Milioni 504, na mradi huo utawanufaisha wananchi wote kwa Ukanda wa Kusini mwa Dar es Salaam yakiwemo maeneo ya Kigamboni, Kibada, Mkuranga, Temeke, Mtoni Kijichi na maeneo mengine yasiyokuwa na mtandao wa maji wa DAWASA kwa ukanda huo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: