Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa hotuba kwa wazee wakati wa kufunga kikao kazi kilichokaa Jijini Dodoma kwa siku mbili kujadili mbinu mpya za kukabiliana na mauaji ya vikongwe lakini pia kujijengea uelewa wa Mkakati mpya wa Kutokomeza mauaji ya Wazee Nchini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa hotuba kwa wazee wakati wa kufunga kikao kazi kilichokaa Jijini Dodoma kwa siku mbili kujadili mbinu mpya za kukabiliana na mauaji ya vikongwe lakini pia kujijengea uelewa wa Mkakati mpya wa Kutokomeza mauaji ya Wazee Nchini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikao mara baada ya kufunga kikao kazi kilichokaa Jijini Dodoma kwa siku mbili kujadili mbinu mpya za kukabiliana na mauaji ya vikongwe lakini pia kujijengea uelewa wa Mkakati mpya wa Kutokomeza mauaji ya Wazee Nchini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akibadilisha na mawazo na Bibi Corotrida Kokupima muda mchache baada kufunga kikao kazi kilichokaa Jijini Dodoma kwa siku mbili kujadili mbinu mpya za kukabiliana na mauaji ya vikongwe lakini pia kujijengea uelewa wa Mkakati mpya wa Kutokomeza mauaji ya Wazee Nchini.

Na Anthony Ishengoma

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameiagiza Idara ya Ustawi wa Jamii kuhakisha inandaa haraka sana Sera ya Wazee kwa kuwa sera iliyopo ni ya siku nyingi na ilianza tangu mwaka 2003 hivyo inatakiwa sera mpya itakayoendana mabadiliko ya sasa.

Aidha Dkt Ndugulile amesema hayo wakati wa hotuba yake ya kufunga kikao kazi kilichokaa Jijini Dodoma kwa siku mbili kujadili mbinu mpya za kukabiliana na mauaji ya vikongwe lakini pia kujijengea uelewa wa Mkakati mpya wa Kutokomeza mauaji ya wazee nchini.

Aidha Dkt. Ndugulile ameitaka Idara ya Ustawi wa Jamii pia kuarakisha mchakato wa kukamilisha mapema mswada wa sheria ya wazee wa nchini ili haki na stahili za wazee zisiwe suala la hiari bali ziweze kutekelezwa kwa mujibu wa Sheria.

Dkt. Ndugulile pia ameitaka Idara ya Ustawi wa Jamii kuzingatia maelekezo aliyoyatoa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa tarehe 29 Januari Mwaka huu wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maofisa Ustawi wa Jamii kukamilisha mapema sheria ya masuala ya ustawi wa jamii Nchini ili ofisi yake iweze kutoa mrejesho kwa ofisi ya Waziri Mkuu juu ya utekelezaji wa suala hilo.

Aidha Dkt. Ndugulile pia ameagiza sambamba na utekelezaji huo pia ameitaka Idara ya Ustawi wa Jamii pia kuharakisha maandalizi ya muundo wa kada ya ustawi wa jamii ambao utaainisha madaraja, kazi na nini watapaswa kufanya suala ambalo pia ni agizo la Waziri Mkuu.

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika maandalizi mapya ya Sera ya Afya nchini suala la wazee limepewa kipaumbele kwa kuzingatia masuala ya tiba kwa wazee na kwa mala ya kwanza Wizara imetambua sayansi ya tiba ya wazee na imetamkwa wazi katika sera ya Afya kwa mantiki hiyo katika Wizara ya Afya kutakuwa na kitengo maalumu kwa ajili ya tiba na afya za wazee.

Wakati huohuo Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Nchini Bw. Rabikira Mushi alimwambia Naibu Waziri Ndugulile kuwa moja ya maazimio ya Kikao kazi hicho kuarakisha mchakato wa kuanzisha mabaraza ya wazee kuanzia ngazi ya kata ili kuwezesha kuundwa kwa Baraza la Wazee la Taifa.

Aidha Bw. Mushi pia aliongeza kuwa azimio jingine la msingi ni kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii juu ya suala la msingi la kuhakikisha jamii inajenga uelewa kuwa suala la kutunza wazee ni jukumu la familia na jamii yake.

Aidha wazee hao pia wameazimia kuwa lazima serikali ihakikishe madirisha ya wazee yanakuwa na dawa muda wote kwani pamoja na uwepo dirisha hilo wakati mwingine madirisha hayo yanakuwa hayana dawa za kutosha kukidhi mahitaji ya matibabu ya wazee.

Aidha wazee kupitia maazimio yao wazee wameiomba serikali kuwapa kipaumbele cha kupatiwa mikopo kama ilivyo kwa makundi mengine tete katika jamii ambayo yanapewa mikopo na serikali kama vile wanawake vijana na walemavu ili nao waweze kujikwamua kiuchumi.

Aidha Kamishna Mushi alisema kuwa wazee pia walipendekeza kuwepo kwa kampeni ya nyumba kwa nyumba, mkono kwa mkono ili kukabiliana na mauaji ya wazee akiongeza kuwa kama kampeni hii ikifanikiwa Maafisa Ustawi wa Jamii wataweza kubaini wazee wote walioko katika hatari kuuawa.

Kikao kazi hiki kimefanyika kufuatia kukamilika na kuzinduliwa kwa Mkakati wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee na uliwakutanisha wawakilishi wazee, Maafisa Ustawi wa Jamii pamoja na Makanda wa Jeshi la Polisi kutoka kanda ya ziwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: