Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mamlaka ya Majisafi na MajiTaka (DAWASA) imesema itaendelea kuwatumia vyema wakandarasi wa ndani ili kuweza kuongeza kasi ya umaliziaji wa miradi kwa wakati.

Miradi inapokwisha kwa wakati wataweza kuwapatia huduma ya Maji wakazi wa Dar es Salaam na Pwani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani, Mkurugenzi wa Manunuzi wa DAWASA Hellen Lubogo amesema kuwa bila kitengo chake kusimama vyema katika kuchakata vyema kupata wakandarasi wenye ubora na kununua vifaa ubora hakika mamlaka inaweza kushindwa kuwapa huduma stahiki wateja.

"Idara yangu ikilegalega katika kupata wakandarasi na vifaa kwa wakati kila kitu kinalala hivyo ni vyema tufanye kazi kwa bidii ili kuifanya mamlaka yetu iweze kuwahudumia vyema wateja wetu," amesema Lubogo.



Miradi hiyo ni Mradi wa Maji SalaSala, Kizudi, Mradi wa Maji Kiembeni, Bagamoyo, Mradi wa Maji Kiwalani hatua ya kwanza na pili, Mradi wa Maji Mkuranga, Mradi wa maji Visima Kimbiji, Mradi wa Maji Jet Buza na mingine mingi.
 Mradi wa Tenki la Maji la Kibamba litakalokuwa likipeleka maji Kisarawe.
 Mradi wa Tenki la Maji la Kisarawe litakalowawezesha wakazi wa Kisarawe na vitongoji vyake.
Mradi wa Tenki la Maji la Kinyerezi.

Amesema Kitengo chao kinafanyakazi kwa kushirikiana na idara nyingine na sasa wamejipanga vyema kukamilisha miradi yote aliyoitaja ili wananchi wa Dar es Salaam na Pwani kupata huduma ya majisafi na salama.

"Idara ya Manunuzi inatumia sheria ya Manunuzi ya mwaka 2016 kutekeleza miradi hiyo kwa kasi kulingana na mahitaji ya mipango tuliyojiwekea ," alisema.

"Niwatoe hofu wananchi mpaka sasa DAWASA haina tatizo la vifaa maana wameweza kupata vifaa vyanye ubora na hivyo wananchi wasipate wasiwasi watapatiwa huduma za maji," amesema.

Ameongeza kuwa kwasasa wanatumia mfumo wa kuwashirikisha wakandarasi wa ndani ili kuweza kuharakisha umaliziwaji wa miradi kwa wakati.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: