MKUU wa wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Zainabu Abdallah akizungumza wakati akifungua warsha ya vijana juu ya kutambua malengo 17 ya  maendeleo endelevu ya Dunia yaliyoendeshwa na serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) yakishirikisha vijana 100 wa kike  na kiume kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Alvaro Rodrigues kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Alvaro Rodrigues akizungumza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kulia ni Mwenzeshaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Didi Nafisa ambaye pia ni Afisa Habari wa Shirika hilo.
Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange akizungumza.
Mwenzeshaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Didi Nafisa ambaye pia ni Afisa Habari wa Shirika hilo akizungumza.
Sehemu ya Vijana kutoka maeneo mbalimbali wilayani Pangani wakifuatilia warsha hiyo kwa umakini.
MKUU wa wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Zainabu Abdallah amesema umaskini hauwezi kuondoka ikiwa vijana bado hawatajituma katika kufanya kazi kwa bidii.

Zainabu aliyasema hayo mjini Pangani wakati akifungua warsha ya vijana juu ya kutambua malengo 17 ya maendeleo endelevu ya Dunia yaliyoendeshwa na serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) yakishirikisha vijana 100 wa kike na kiume.

Alisema lazima vijana watambua upo umuhimu wa kutumia fursa zilizopo kwenye maeneo yao badala ya kukaa na kuacha kufikiria kukaa vijiweni na kujiingia kwenye makundi yasiyokuwa na tija kwa maendeleo.

“Matatizo ya vijana wanayafahamu vijana hivyo serikali ipo tayari kuwaunga mkono kwa juhudi zozote mnatakazo anzisha …lakini pia mwaka huu kuna chaguzi za serikali za mita hivyo tunataka viongozi vijana tutakaoweza kuzungumza nao lugha moja na kusimamia maendeleo endelevu ya dunia”Alisema.

Aidha alisema kupitia mafunzo hayo yatasaidia kuongeza wigo mpana wa fursa kwa vijana wilayani humo ambao watakwenda kuibadilisha wilaya hiyo na kuwataka wazazi kuhakikisha wanawapatia elimu bora watoto waop badala ya kujiingiza kwenye shughuli za uvuvi.

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka vijana wa Pangani kuchangmkia fursa hiyo ili iweze kuwasaidia ikiwemo kujitambua kwamba wana nafasi gani kwa Taifa na wilaya kwa kujiletea maendeleo kwani wao ndio chachu ya mafanikio kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kiuchumi, kisiasa na kujamii.

Awali akizungumza wakati wa warsha hiyo Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Alvaro Rodrigues alisema uwepo wao ni kwa ajili ya kutekeleza malengo endelevu ambayo ndio malengo ya dunia 2016 hadi 2030 kwa kuwapatia elimu vijana ili wawezi kujitambua na kuona namna ya kutumia fursa zilizopo kwenye maeneo yao.

Alisema pia kwenye mafunzo hayo wanajikita kuwasaidia wanawake kutokana na kwamba asilimia 50 ya watu duniani ni wanawake hivyo wakiachwa nyuma dunia inaweza kudhoofisha maendeleo.

“Nusu ya idadi ya watu dunia ni wanawake hivyo ikiwa wataachwa nyuma kwenye Nyanja zote za kimaendeleo maanake tutakuwa tumerudisha nyuma ukuaji wa uchumi kwa wananchi”Alisema

Hata hivyo alisema ifikapo 2030 wawe na ulimwengu bora kwa kuzingatia malengo ya milenia katika kuhakikisha vijana wanazingatia malengo ya maendeleo endelevu ambayo ni watu, sayari, ustawi, amani na ushirikiano.

Kwa upande wake Mwenzeshaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Didi Nafisa aliwataka vijana walioshiriki kwenye warsha hiyo kuzingatia mafunzo hayo ili yaweze kuwa na tija ikiwemo kubadilisha maisha yao.

Nafisa ambaye pia ni Afisa Habari wa Shirika hilo alisema mafunzo hayo yatasaidia kuwakwamua vijana na tatizo la ukosefu wa ajira ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa nchi nyingi dunia.

“Tatizo la ukosefu wa kazi dunia linaongezeka kutoka watu milioni 170 kwa mwaka 2007 hadi kufikia milioni 202 mwaka 2012 hapo utaona sasa watu milioni 75 kati ya hao ni vijana wa kike na kiume”Alisema
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: