Rais mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha (UDSM ) akizungumza kwa msisitizo na uongozi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Ndaki ya Afya na Sayansi Shiriki (UDSM -MCHAS) katika ziara yake ya kutembelea na kukagua eneo kitakapo jengwa Chuo katika eneo la Tanganyika Pekers nje kidogo ya Jiji la Mbeya .

Rais mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha (UDSM ) akiwa na Shangazi yake Marehemu Efraemu Kibonde Elinelia Kibonde baada ya kumkuta akiwa katika foleni ya kusubiri Matibabu katika dirisha la dawa la Bima ya Afya katika Hospital ya rufaa ya Kanda Mbeya. Picha na Emanuel Madafa Mbeya.
Rais mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha (UDSM ) akiwa na wanafunzi wa udaktari kitengo afya ya meno Chuo kikuu cha Dar es Salaam Ndaki ya Afya na Sayansi shiriki (UDSM -MCHAS) katika ziara yake ya kutembelea na kukagua eneo kitakapo jengwa Chuo katika eneo la Tanganyika Pekers nje kidogo ya Jiji la Mbeya .
Rais mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha (UDSM ) katikati walioketi akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Ndaki ya Afya na Sayansi shiriki (UDSM -MCHAS) mara baada ya kuzungumza nao.
ais mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha (UDSM ) aliyeweka mkono mfukoni akiwa na uongozi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Ndaki ya Afya na Sayansi shiriki (UDSM -MCHAS) wakiwa eneo la chuo katika ziara yake ya kutembelea na kukagua eneo kitakapo jengwa Chuo katika eneo la Tanganyika Pekers nje kidogo ya Jiji la Mbeya nyuma yake ni Mwenyekiti wa baraza la hicho Jaji Mstaafu Damian Luguva.


Na Emmanuel Madafa.


MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rais Mstaafu awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amewataka watendaji wa Chuo hicho kusimamia nidhamu na ubora wa elimu ili kiwe chuo cha mfano Barani Afrika.

Rais, Kikwete aliyasema hayo jana wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa chama na serikali, baada ya kutembelea na kukagua eneo la ardhi lililotengwa na serikali ya Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho Ndaki ya Afya na Sayansi Shiriki (MCHAS).

Amesema, shabaha yao nikuongeza nguvu ya wataalamu nchini, hivyo watendaji wanawajibu wa kusimamia kiwango cha elimu kinachotolewa hakishuki na kamwe hatapenda kuona watu wa bora liende wakikiendesha chuo hicho.

“Sipendi kuona sifa hii ya elimu bora ikishukia Mbeya, sipendi kuwaona watu wanaosema bora liende tu, madaktari ni watu muhimu sana kwani wanashindana na uhai wa mtu usiondoke, hivyo sitaki kuona mchezo ukifanyika,”alisema.

Aidha, akijibu agizo hilo Naibu Makamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Bonaventure Rutinwa, amesema kamwe hatakubali mtumishi au mwanafunzi yoyote kuharibu sifa ya chuo chuo hicho ambacho kimebahatika kutoa viongozi wakubwa watano wa Afrika.

“Chuo hiki kimewatoa viongozi wakubwa akiwemo Rais Magufuri, Rais wa Uganda Yower Kaguta Museven, Rais wa sasa wa Malawi, Bingu wa Mutarika, Rais Mstaafu wa Tazania awamu ya nne, Jakaya Kikwete, Rais wa awamu ya tatu Tanzania, Benjamin Mkapa na Rais wa zamani wa Sudan Kusini Dr. John Mabior,”alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: