Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni moja mfanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2018/2019 (Novemba 2018 – Januari 2019) Afisa Uuguzi Prisca Kiyuka wakati wa hafla fupi ya kumpongeza iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Prof. Mohamed Janabi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi Afisa Uuguzi Prisca Kiyuka cheti cha kutambua utumishi wake baada ya kuwa mfanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2018/2019 (Novemba 2018 – Januari 2019) katika hafla fupi ya kumpongeza iliyofanyika leo katika ukumbi wa taasisi hiyo uliopo Jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi Robert Mallya na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Fedha Mohamed Songoro.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye ni mfanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2018/2019 (Novemba 2018 – Januari 2019) Prisca Kiyuka akitoa neno la shukrani wakati wa hafla fupi ya kumpongeza ilioyofanyika leo katika ukumbi wa taasisi hiyo uliopo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Yeyeye akimpongeza mfanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2018/2019 (Novemba 2018 – Januari 2019) Afisa Uuguzi Prisca Kiyuka wakati wa hafla fupi ya kumpongeza iliyofanyika leo katika ukumbi wa taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Utawala Joachim Asenga. Picha na: JKCI.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: