Mwili Wa marehemu Ruge Mutahaba tayari umekwisha wasili nyumbani kwao kijijini Kiziru Bukoba mkoani Kagera leo,ambapo watu mbalimbali wamejitokeza kumpokea,huku msafara huo ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti.
Sanduku lenye mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba ukipokelewa uwanja wa ndege wa Bukoba 'Bukoba Airport',na kupokelewa na watu mbalimbali huku Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akiongoza mapokezi hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Brigedia Jenerali Marco Gaguti amefika uwanja wa ndege kuongoza mapokezi ya mpendwa wetu Ruge Mutahaba. Kabla Brigedia Jenerali Marco Gaguti kufika hapa Kagera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kipindi kile alikuwa ni Kanali kabla ya kupanda cheo amefanya kazi za kizalendo bega kwa bega na Ruge Mutahaba mojawapo ikiwa ni Fursa na Ile ya Umoja wa Mataifa Kigoma Programu ya pamoja.
Wazazi wa Marehemu Ruge,Prof Mutahaba na Mkewa akiwasili uwanja wa ndege wa Bukoba.
Mtoto wa kwanza wa Marehemu akifarijiwa baada ya kuwasili Bukoba.
Sanduku lenye mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba likipokelewa uwanja wa ndege wa Bukoba 'Bukoba Airport',na kupokelewa na watu mbalimbali huku Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akiongoza mapokezi hayo.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: