Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imewatambua waandishi sita wanawake ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika halmashauri hiyo kupitia taarifa mbalimbali wanazoziandika. Waandishi hao ni Nora Damian (Mtanzania), Eva Sosoko (TBC 1), Futuna Seleman (ITV), Lucy Ngowi (Habari Leo), Beatrice Erick (Channel Ten) na Cecilia Jeremiah (Uhuru Fm).(pichanani Nora Damian akipokea cheti kutoka kwa Meya wa Manispaa Ilala Charles Kuyeko (Katika anayeshuhudia tukio hilo Ofisa Uhusiano Ilala Tabu Shaibu.
Nora Damian ametambuliwa kupitia makala ya elimu aliyoiandika ambayo ilihusu changamoto za uhaba wa vyoo katika shule mbalimbali za halmashauri hiyo na makala hiyo imeiwezesha halmashauri kuja na mpango wa ujenzi wa choo maalumu cha mtoto wa kike katika kila shule ambacho kitamuwezesha mtoto wa kike hata anapokuwa katika hedhi kuweza kuhudhuria masomo bila shaka yoyote, hadi sasa halmashauri imeshajenga vyoo vitatu na mpango ni kujenga katika shule zote. (PICHA NA HABARI HERI SHAABAN)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: