Mke wa Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Asha Suleiman Idd katika akiwa kwenye halfa hiyo kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu, Stella Ikupa kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye dhifa ya chakula cha mchana kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mabweni maalum kwa ajili ya watoto wenye ulemavu.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga akizungumza wakati wa halfa hiyo.
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa halfa hiyo.
MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Nassib Mbaga akizungumza katika halfa hiyo.
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Mama Asha Seif Iddi kulia akimtazama mtoto mwenye ulemavu wa viungo Maimuna Yahaya anayesoma shule ya Msingi Bagamoyo wilayani Muheza akikata keki kwa mdomo wakati wa halfa hiyo ya kuchangia watoto wenye mahitaji maalumu kwa kujenga mabweni ya wanafunzi wenye ulemavu na vifaa vya mahitaji hayo uliofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo.
Mke wa Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Asha Suleiman Idd kulia akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa kwa kwanza kulia kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo mara baada ya kukagua mabanda mbalimbali vya kwenye dhifa hiyo.
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda kushoto akimvalisha kofia mtoto mwenye ulemavu wa ngozi wakati wa dhifa hiyo.
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda kulia akipewa mkono na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Nassib Mbaga mara baada ya kumaliza kutoa hotuba yake wakati wa halfa hiyo.
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa kushoto akimkabidhi baiskeli mtoto mlemavu wilayani Muheza kwa ajili ya kumsaidia kuenda n ayo shule kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo.
Mke wa Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Asha Suleiman Idd kushoto akisalimiana na viongozi mbalimbali wilayani Muheza mara baada ya kuwasili kwa ajili ya halfa ya chakula cha mchana kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mabweni maalum kwa ajili ya watoto wenye ulemavu kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Moyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo.
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenye ulemavu,Stella Ikupa kushoto akisalimia na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jitegemee kwa ajili ya halfa hiyo.
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kushoto wakiteta jambo mara baada ya kuwasili kwenye halfa hiyo.
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Nassib Mbaga wakati wa halfa hiyo kulia ani Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu.
PRO wa Bandari ya Tanga Moni Jarufu akifuatilia matukio mbalimbali kwenye halfa hiyo.
Mwalikishi wa Bandari Tanga akiwa kwenye Halfa hiyo.
Sehemu ya wadau wa elimu akiwemo Nassoro Makau ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers akiwa kwenye halfa hiyo.
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Asha Suleimani Iddi ameongoza harambee maalumu ya kuchangia ujenzi wa mabweni maalumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wilayani Muheza huku akiitaka jamii kubadilika na kuhakikisha watoto hao wanapelekwa shulen ili kupata elimu.

Alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa dhifa ya chakula cha mchana kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mabweni maalum kwa ajili ya watoto wenye ulemavu ambapo alisema unyanyapaa, mazingira yasiyo rafiki katika shule imeelezwa kuwa ni miongoni mwa sababu za watoto wenye ulemavu kushindwa kupelekwa shule kwa ajili ya kupata haki yao ya kielimu.

Alisema kuwa bado jamii haijapa mwamko mkubwa wa kutoa fursa ya kuwapatia elimu watoto wenye ulemavu hali inayosababisha wengi wao kubaki majumbani tu.

Alisema kuwa licha ya serikali kufanya jitihada kubwa za kuboresha mazingira ya kielimu katika maeneo mbalimbali lakini bado kundi hilo nlimekuwa likikabaliwa na changamoto ikiwemo uhaba wa vifaa visaidizi vya  kuwawezesha kusoma.

Aidha alisema mkakati huo wa ujenzi wa mabweni wilayani humo utaweza kutoa fursa kwa watoto wengi wenye ulemavu kupata haki yao ya kusoma bila ya kuwepo kwa vikwazo vya namna yoyote ambavyo vilikuwepo hapo mwanzoni

Hata hivyo aliwataka wazazi na walimu kuhakikisha wanawalinda watoto hao dhidi ya vitendo vyote viovu ikiwemo ubakaji pamoja na uzalilishaji wa kijinsia.

Mama Asha alisema kuwa mara tuu baada ya mabweni hayo kukamilika wazazi wanajukumu la kuhakikisha wanawatoawatoto hao na kuwapeleka shule kwa ajili ya kupata elimu badala ya kuwaficha.

Katika hafla hiyo Mke huyo wa Makamu wa Pili wa Rais SMZ Asha alimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kiasi cha sh.milio sita (6000,000).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: