Mtangazaji wa Clouds FM Ephrahim Kibonde (Pichani) amefariki dunia jijini Mwanza.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amethibitisha kufariki kwa mtangazaji huyo kutokana na kusumbuliwa na presha.

Imeelezwa kuwa Kibonde alianza kusumbuliwa na Presha tangu akiwa Bukoba kwenye msiba wa Marehemu Ruge Mutahaba na baadae akahamishiwa Mwanza kwa uangalizi zaidi.

Aidha Mkuu wa vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga amethibitisha kufariki Dunia kwa Ephrahim Kibonde leo asubuhi katika hospitali ya Bugando, Mwanza.

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa jina la Bwana libarikiwe.

'Maisha haya ni mafupi ... Ukipata nafasi ya kumwambia mtu unampenda mwambie,akiumwa kampe pole,akikuomba msamaha samehe... ukimkumbuka mjulie hali..Usiyape majivuno nafasi, tuna muda mchache duniani'...

'Uhai ni zawadi, kifo ni lazima... huu ujumbe utakusaidia sana kwenye Maisha yako'
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: