Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars ambao walifika Ikulu mara baada ya kufanikiwa kufuzu kushiriki Fainali za michuano ya Mataifa ya Africa AFCON baada ya kuifunga Timu ya Taifa ya Uganda The Cranes magoli 3-0 jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars waliopo upande wa kulia pamoja na viongozi wengine wakionesha ishara ya magoli matatu ambayo timu ya Taifa iliupata siku ya jumapili zidi ya Timu ya Taifa ya Uganda The Craines na kufanikiwa kufuzu kucheza Fainali za michuano ya Mataifa ya Africa AFCON nchini Misri baadae mwaka huu.

Na Emmanuel J. Shilatu.

1. Ukimulika idara ya michezo unaiona Taifa Stars ikifuzu AFCON Mwaka huu tangu mara ya mwisho 1980; Kule bondia Mwakinyo akiwakilisha vyema kwenye masumbwi.

2. Ukitazama angani unaona ndege 6 ikiwemo ya Dreamliner ikikata mawimbi nchini na anga za Kimataifa zikiongeza Watalii nchini, zikiimarisha usafiri wa anga na kuongeza mapato.

3. Ukienda sekta ya Elimu unakutana Tanzania ya Leo inatoa Elimu bure kuanzia Shule ya msingi Hadi Sekondari. Pia ikitoa mikopo kwa kiwango kikubwa na idadi kubwa ya wanufaika kwa Wanazuoni.

4. Ukienda sekta ya madini unakutana na mikataba mipya ya madini yenye tija kwa Taifa, Mererani unakutana na ukuta unaozuia madini yetu kuibwa. Siku hizi raha hata mchanga wa madini hausafirishwi tena nje ya nchi.

5. Ukienda sekta ya usafirishaji unakutana na ujenzi wa reli ya kisasa SGR ambapo Watanzania wataokoa rasilimali muda na fedha kwa treni hii ya umeme.

6. Ukienda sekta ya miundombinu utakutana na daraja la Tazara likitumika, daraja la Ubungo na la Surrender yakijengwa; Usichoke nenda ukaone barabara ya kutoka Morocco mpaka Mwenge yenye njia 6 ikitumika huku ya Ubungo ikiendelea ujenzi wa njia 6. Hapo sijayataja madaraja ya Furahisha, ya Kilombero n.k yakiwa yamekamilika.

7. Ukienda Dodoma utajionea mwenyewe Serikali ilivyohamia Dodoma. Siku hizi Dar imebaki kuwa jiji la kibiashara.

8. Ukienda sekta ya umeme utakutana na miradi mikubwa ya Kinyerezi K-1 extension na KII ikitumika. Usisahau kutazama mto Rufiji kuna ujenzi wa Stiglers utakaozalisha Megawats zaidi ya 2100.

9. Ukienda sekta ya afya utakutana na majengo ya kisasa, wahudumu, dawa na vifaa tiba vya kisasa kabisa. Siku hizi hauhitaji kwenda nje kutibiwa kwani operation kubwa za afya zinafanyika hapa hapa nchini.

10. Kwenye sekta ya uchumi napo tupo vizuri, kwa wale wanaojituma kufanya Kazi watakubliana nami kuwa Kodi nyingi sumbufu na kero zimefutwa; Uchumi Sasa unakuwa kwa wastani wa 7.2 ; Ujenzi wa miundombinu ya reli, barabara, madaraja unaiweka Tanzania kwenye nafasi nzuri ya ukuaji na uimarikaji wa uchumi wetu zaidi kwa siku zaidi.

11. Ukienda sekta ya Watumishi, siku hizi kuna nidhamu na uwajibikaji wa hali ya juu. Hali hiyo imesababisha kiwango cha rushwa na ufisadi kipungue sana nchini.

12. Ukienda popote pale nchini unakutana na Tanzania ya Viwanda ambapo sasa vipo zaidi ya 3000 nchini. Pia ukikatiza Geita utakutana na soko la kwanza la madini ya dhahabu Tanzania na la tatu Afrika. Hii Ndio Tanzania mpya na ya mfano.

Shilatu E.J
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: