Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa duka jipya la Tigo lililopo mtaa wa Miomboni mjini Iringa, akiwatubia wananchi waliofika katika uzinduzi wa tawi hilo linaloweza kuwahudumia wateja wengi Zaidi kwa wakati mmoja
 Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduziwa duka jipya la Tigo lililopo mtaa wa Miomboni mjini Iringa, akikata utepe kuashiri uzinduzi rasmi wa duka hilo litakalokuwa na uweza wa kuwahudumia wateja wengi zaidi.
  Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduziwa duka jipya la Tigo lililopo mtaa wa Miomboni mjini Iringa, akiwa na Abbas Abrahmani ambaye ni Meneja wa Tigo kanda ya Kusini pamoja na Laverty Khana ambaye ni Meneja Huduma kwa Wateja kanda ya Kusini muda mfupi kabla ya uzinduzi rasmi wa duka hilo
  Mgeni rasmi kwenye tukio la uzinduzi wa duka jipya la Tigo lililipo mtaa wa Miomboni mjini Iringa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela (wa kwanza kulia) akipata maelekezo kutoka kwa wafanyakazi wa Tigo namna wanavyohudia wateja.
Waandishi wa habari wakichukua matukio mbali mbali ikiwamo hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela kwenye uzinduzi wa duka jipya la Tigo lililopo mtaa wa Miomboni mjini Iringa

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya Tigo leo imezindua duka jipya la huduma kwa wateja lililopo Iringa mjini ambalo litarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wake wa eneo la Iringa mjini na maeneo ya jirani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo Mkurungezi wa kanda ya Kusini wa Tigo, Henry Kinabo, amesema tawi hilo jipya lililopo mtaa wa Miyomboni, ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo kuwafikishia wateja wake huduma zake karibu zaidi.

Kinabo alisema duka hilo litahudumia wateja zaidi ya 100 kwa siku kwa kuwapa huduma mbalimbali za Tigo ikiwemo huduma ya kuunganishwa na intaneti, usajili wa laini za simu, Tigo Pesa na huduma za simu janja.

“Duka hili lina manufaa makubwa kwa wateja kwa sababu imepeleka huduma zetu kuwa karibu zaidi na wao. Pia linapatikana sehemu nzuri inayofikika kirahisi kiasi kwamba litavutia wateja wengi kutoka maeneo jirani. Tumebadilisha pia muonekano wa duka letu kuwa mzuri zaidi, na kuongeza pia nafasi ili kuweza kuwahudumia wateja wengi zaidi kwa wakati mmoja,” alisema.

Aliongeza, “Kupitia duka letu hili lililoboreshwa, wateja watapata pia promosheni zetu mbali mbali kama; 4G+, App ya Tigo Pesa, promosheni ya CASH IN kwa mawakala, pamoja na simu mpya za S10 na S10+.”

Duka hili limetenga pia sehemu maalum ya uuzaji wa bidhaa mbalimbali kama simu janja ambapo mteja anaruhusiwa kuzijaribu kabla ya kununua. “Hii inamuwezesha mteja kufanya uamuzi sahihi kabla ya kununua, hivyo huchagua na kununua aina ya simu inayokidhi mahitaji yake.”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: