Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Joketi Mwegelo akizungumza katika maadhimisho ya Siku Kutenda Mema iliyofanyika viwanja vya Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa VPCO Emmanuel Makundi akizungumza kuhusiana na maadhimisho ya siku ya kutenda mema na mchango wa wadau mbalimbali yaliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Vijana wakichangia Damu katika maadhimisho ya Siku Kutenda Matendo mema yaliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Mkoa wa Dar es Salaam Mariam Juma akizungumza hali ya uchangiaji wa damu katika maadhimisho ya Siku ya Kutenda Mema iliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco Jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja wakitangaza amani katika maadhimisho ya siku ya kutenda matendo Mema iliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco jijini Dar es Salaam.


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.


Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Joketi Mwegelo amesema kuwa ukuta kwa vijana ni kutenda matendo yaliyo mema ikiwemo kusaidia au kutoa msaada pale penye uhitaji, wakati wa Maadhimisho ya Siku Kutenda Mema 'Good Deeds Day' iliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco Jijini Dar es Salaam.

Amesema hata vitabu vya Mungu vinafundisha kutenda mema ikiwemo kutoa pale panapohitajika na mafanikio yake yataonekana kwa kile ambacho mtu anajitoa. Mwegelo amesema hata yeye katika harakati zake vijana wenzake wamekuwa na mchango mkubwa wa kujitoa bila kuangalia maslahi ya kifedha.

Aidha amesema kuwa maadhimidlsho ya siku ya kutenda mema iwe ni njia ya jamii kuangalia vitu vya kufanya katika kusaidia watu wengine.

Naye Mwenyekiti wa VPCO na Mratibu wa Maadhimisho hayo, Emmanuel Makundi amesema kuwa wameandaa maadhimisho kwa kutambua matendo mema ndio nguzo ya amani, na matendo mema ni pamoja kuhakikisha kila mmoja anaishi kwa amani.

Makundi amesema wamefanya mambo mbalimbali ya jamii na watu wamekuwa na mwitikio katika kuwaunga mkono wa kusaidia watu wengine.

Afisa Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Mkoa wa Dar es Salaam, Mariam Juma amesema kuwa mahitaji ya damu kwa nchi ni chupa laki tano lakini ukusanyaji umefikia laki tatu hivyo wanahitaji wananchi wajitokeze katika kuchangia damu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: