Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akizindua Mkataba wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo leo Aprili 12,2019 Jijini Dodoma. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Katibu Mkuu Bibi Susan Mlawi ( wa pili kushoto) ,Naibu Katibu Mkuu Bw.Nicholas William (wa pili kulia),Katibu wa Baraza hilo Bw.Bernad Lubogo (wa kwanza kulia) pamoja na Mwenyekiti wa TUGHE Tawi Bibi.Magreth Mtaki ( wa kwanza kushoto).
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo leo Aprili 12,2019 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo leo Aprili 12,2019 Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kuzindua Mkataba wa Baraza hilo leo Aprili 12,2019 Jijini Dodoma.

Na Shamimu Nyaki-WHUSM, DODOMA.

Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watumishi wa wizara hiyo kutimiza wajibu wao katika kutekeleza majukumu ya kila siku ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kutatua kero na kujibu hoja za wananchi kwa ufanisi na haraka.

Hayo ameyasema leo Jijini Dodoma alipokuwa akifungua Baraza Jipya la Wafanyakazi wa wizara hiyo ambalo hukutana mara mbili kwa mwaka kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayohusu utendaji na maslahi ya watumishi.

“Napenda kusisitiza kuwa vikao vya baraza la wafanyakazi vitumike kujadili malengo na mipango ya wizara ikiwa ni pamoja na maslahi ya watumishi ” Dkt. Harrison Mwakyembe

Ameongeza kuwa mabaraza ya wafanyakazi yapo kwa ajili ya kujadili utendaji wa kila siku na jinsi ya kuboresha zaidi utendaji huo unaolenga kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi.

Aidha Dkt. Mwakyembe amewaagiza Wakuu wa Idara na Vitengo kusimamia kwa dhati suala la maadili katika sehemu za kazi kwa kuhakikisha watumishi wanatumia muda wa kazi vizuri kuwahudumia wananchi.

Kwa Upande wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi amewakumbusha watumishi kushiriki kikamilifu na kuwa mstari wa mbele katika kupambana na VVU/UKIMWI.

“Ugonjwa wa UKIMWI unagharimu Taifa hivyo nasisitiza kuwa kiini cha ufanisi katika vita hii ni kwa kila mmoja wetu kubadili tabia” Katibu Mkuu Bibi. Susan Mlawi.

Pia amewasisitiza watumishi hao kufanya kazi kwa weledi ,bidii na tija kwa kuwa hakuna haki bila wajibu.

Naye Mwenyekiti wa TUGHE Tawi Bibi Magreth Mtaki amesema kuwa Baraza la Wafanyakazi linasaidia wafanyakazi kujadili na kuboresha utendaji kazi wa Wizara ili kuleta maendeleo ya Taifa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: