Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Umma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dr. Arnold Towo akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Mt. John Paul II ya Kahama Mkoani Shinyanga walipofanya ziara ya masomo kwa vitendo katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam tarehe 12 Aprili, 2019.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mt. John Paul II ya Kahama Mkoani Shinyanga wakisikiliza kwa makini kuhusu huduma zinazotolewa na Chuo kikuu cha Dar es Salaam wakati wa ziara waliyofanya katika Kitengo cha Huduma kwa Umma.
Bi Elizabeth Chuwa kutoka Kurugenzi ya Masomo ya Shahada ya Awali akiwaeleza wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mt. John Paul taratibu za kujiunga na chuo Kikuu cha Dar es salaam wakati wa ziara fupi iliyofanywa na shule hiyo ikiwa ni sehemu ya kujifunza kwa vitendo katika Kitengo cha Huduma kwa Umma cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kifaa cha Kisasa cha Kutunzia kadi za Kielektroniki ( Electronic Cabinet ) chenye kadi 170 kilichopo katika Maktaba Mpya ya Kisasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mwandamizi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ernest Nyari akiwaelekeza wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mt. John Paul ya Kahama namna kabati la Kielektroniki linavyotumiwa na wanafunzi wanapoingia Maktaba wakati wa kujisomea.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mt. John Paul wa II wakiwa wamekaa ndani ya chumba kisasa cha taarifa za mtandaoni " Online Publications" wakati wa ziara fupi ya masomo kwa vitendo iliyofanywa na shule hiyo katika Kitengo cha Huduma kwa Umma cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Msaidizi wa Maktaba Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Dickens Dominic akiwafafanulia jambo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya John Paul II wakati wa ziara ya kimasomo waliyofanya kujionea namna Maktaba mpya inavyofanyakazi.
Mkurugenzi Mwandamizi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ernest Nyari akiwaonesha wanafunzi (Hawapo pichani) moja ya Vitabu vya Sayansi vinavyopatikana katika chumba cha Maktaba mahususi kwa ajili ya masomo ya Sayansi kiitwacho " Science Collection" wakati wa ziara fupi iliyofanywa na shule ya Sekindari ya Mt. John Paul II katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Umma ( Mwenye shati la Bluu) pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitengo cha Huduma kwa Umma na Maktaba Mpya wakiwa katika Picha ya Pamoja na Wanafunzi na walimu kutoka Shule ya Sekondari ya Mt. John Paul II kutoka Kahama Shinyanga baada ya ziara fupi katika Maktaba hiyo.
---
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Umma Dk. Arnold Towo amewaeleza wanafunzi wa Kidato cha I hadi 6 wa Shule ya Sekondari ya Mt. John Paul II kutoka Kahama Mkoani Shinyanga kuzingatia vema masomo yao ili kuwa na msingi bora wa elimu na kuweza kuchagua masomo yao vema ili kukidhi mahitaji yao wanapofikia hatua ya kujiunga katika Masomo ya Shahada za juu.

Amesema hayo wakati wa ziara fupi iliyofanywa na uongozi wa shule ya Mt. John Paul II pamoja na wanafunzi 55 walipotembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kujifunza kwa vitendo na kufahamu utendaji kazi wa Chuo Kikuu Mlimani.

"Napenda kuwasisitiza wanafunzi kutumia muda wao vema wa masoma, kujituma na kujifunza vitu tofauti pamja na kutambua mapema kile unachotaka kusomea ili inapofika wakati wa kujiunga na chuo kikuu wawe wamejitambua na kufahamu vema wanataka kusoma nini, alisisitiza Dr. Towo.

Miongoni mwa vitu walivyojifunza wakati wa ziara ni pamoja na kufahamu taratibu na vigezo vya kujiunga na Chuo kikuu cha Dar es Salaam kutoka kurugenzi ya masomo ya Shahada ya awali, masuala ya uhandisi wa umeme na kupata kupata ufafanuzi kuhusu masuala ya historia ya Afrika pamoja na kutembelea na kuona jinsi maktaba mpya inavyofanyakazi.

Dr. Towo aliongeza kuwa, kikubwa katika masomo wanafunzi wanatakiwa kuwa na ujuzi wa juu na ufaulu bora na wenye uwezo wa kujieleze ili kukidhi hitaji la soko pale wanapohitimu masomo yao ya juu.

"Lengo kuu la ziara hii kwa wanafunzi wetu ni kuwajengea uwezo na kuona kwa vitendo yale wanayosikia kuhusu chuo kikuu cha Dar es Salaam pamoja ikiwa ni sehemu ya kuwapa hamasa ya kujituma katika masomo pale wanaporejea shuleni", alisema Mwalimu Enock Julius.

Chuo Kikuu Cha Dar es salaam kinatoa huduma kuu tatu ambazo ni Kutoa Elimu, Kufanya Tafiti pamoja kutoa huduma za ushauri kwa Mashirika ya umma pamoja na Sekta binafsi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: