Na Agness Francis, Blogu ya Jamii

MWENYEKITI wa klabu ya Simba Mohammed Dewji amewasihi mashabiki wa klabu hiyo kuwa washangilie mwanzo mwisho siyo kushangilia mpaka wapate goli katika mechi inayotarajiwa kuchezwa kesho majira ya saa kumi jioni katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ambapo klabu ya Simba SC itaminyana na klabu ya TP Mazembe katika mchezo wa robo Finali ya kuwania kombe la ubingwa barani Afrika. 

Dewji amezungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam ambapo amewaomba sana mashabiki hao kuwa ikitokea bahati mbaya wamefungwa basi waendelee kushabikia sio tu mpaka wakipata goli pia amewasihi wabadilike kwenye hilo, washangilie Simba mwanzo hadi dakika 90 za mpira zitakapomalizika. 

Hata hivyo Kufuatia mechi hiyo Mo amewawaomba mashabiki wa Simba na Watanzania kijitokeze kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao ili wachezaji wapate nguvu na maroli ya kufanya vizuri. 
.
"Kujitokeza kwa mashabiki kuna faida kuu mbili, moja unawaongezea nguvu wachezaji wetu na wao wanaona kuwa Watanzania wapo nyuma yao, lakini pili inawaogopesha wapinzani wetu" amesema Mo Dewji.

"Hapa hatushiriki tu, tunajiamini kwamba tunaweza na tunataka kwenda mbali zaidi ya hapa"amesema Mo. 

Ameongezea kwa kusema kuwa "Shabaha yetu sio tu kufanikiwa mwaka mmoja, tunataka kushinda kombe kila mwaka ili tushiriki Ligi ya Mabingwa kila mwaka, tunataka kushinda kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika, mimi naamini uwezo tunao, tumtangulize Mungu"amesema Dewji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: