Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Bi. Swaum Said Ngenje akielezea kuhusu matatizo aliyoyapata mtoto wake, alipokuwa akihotubia Maelfu ya Wananchi wa Jiji la mbeya waliojitokeza kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya Aprili 26, 2019.
---
Rais Magufuli ameagiza Jeshi la Polisi mkoani Songwe kuanza kuchunguza upya madai ya mtoto wa miaka minne wa kiume kulawitiwa.

Rais ametoa maagizo hayo baada ya mmoja aliyekuwa katika mkutano wa Rais kupata nafasi ya kuzungumza mbele take ambapo alitoa malalamiko ya mtoto wake kulawitia.

Mama huyo baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza amemwambia Rais Magufuli kuwa mtoto wake wa kiume amelawitiwa na sasa anajisaidia muda wote na baada ya kitendo hicho aliamua kwenda kwenye vyombo vya ulinzi na usalama lakini hadi sasa haana msaada wowote zaidi ya kuzungushwa.

Amesema kuwa amekwenda kuonana na Kamanda wa Polis Mbeya,Mkuu wa Jeshi la Polisi ncbini IGP pamoja na Jaji Mkuu lakini anaona anazungushwa tu,hivyo matumaini yake yamebaki kwa Rais Magufuli ambaye ni Rais wa wanyonge.

"Rais wangu naomba msaada wako, nimekwenda kila mahali hadi kwa Jaji Mkuu,nisaidie mheshimiwa Rais ,nyaraka za note ambako nimekwenda ninazo.Mtoto aliyelawitiwa ni mwanaume na picha yake ninayo,lakini kwenye makaratasi wanasema ni mwanamke," amesema mama huyo wakati anamuleza Rais.

Hata hivyo Rais alimuuliza kama amekwenda na mtoto huyo mkutano hapo lakini mama huyo akajibu ameshindwa kwenda naye kwani anajisaidia Mara kwa mara,hivyo hakuweza kufika naye

Kutokana na maelezo hayo Rais Magufuli alimhakikishia mama huyo kuwa uchunguzi utafanyika na haki itatendeka ambapo ameomba nyaraka akabidhiwe mwanasheria ili kuanza ufuatiliaji.

Pia Rais Magufuli alitoa maagizo kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha mama huyo hasumbuliwi huku akimpa fedha kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kujikimu na mtoto wake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: