Kikosi cha Simba SC kilichoanza leo dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo.
Kikosi cha TP Mazembe ya DR Congo kilichoanza leo mchezo dhidi ya Simba SC ya Tanzania. (Picha na Mohammed Ibrahim).
Mashabiki wa Simba SC walifika kushuhudia mchezo huo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Beki wa Kimataifa wa Uganda na Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, Joseph Ochaya akifurahia jambo na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda anayecheza Simba SC ya Tanzania, Meddie Kagere, wakati wa mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Mazembe na Simba, mchezo umemalizika kwa sare ya 0-0 kwenye dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Beki wa TP Mazembe, Joseph Ochaya akijaribu kumtoka Beki wa Simba SC, Zana Coulibaly katika mchezo ulimalizi uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa sare ya 0-0. Timu hizo zitarudiana tena wiki ijayo, April 13, 2019 mjini Lubumbashi nchini Congo.
Dua zikiendelea.
Kiungo wa Simba SC, Haruna Niyonzima akimtoka Mchezaji wa TP Mazembe ya DR Congo kwenye mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mchezo ulimalizika jioni ya leo kwa sare ya 0-0.
Mashabiki wa TP Mazembe ya DR Congo wakifuatilia mchezo huo.
Nyota wa TP Mazembe, Rianford Kalaba akiondoka na mpira wakati wa mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Mazembe na Simba SC, timu hizo zimetoka sare ya 0-0 kwenye dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: