Mkurugenzi mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye (kushoto) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo na anayesikiliza pembeni ni Mjumbe wa bodi TPSF Balozi Abdulsamad Abdulrahimu ambaye pia ni kaimu mwenyekiti wa chama cha watoa huduma sekta yagesi na mafuta.
Mjumbe wa bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi, (TPSF), Balozi Abdulsamad Abdulrahimu ambaye pia ni kaimu mwenyekiti wa chama cha watoa huduma sekta ya gesi na mafuta akizungumza wakati wa mkutano uliokutanisha makampuni makubwa ya wawekezaji katika sekta ya Mafuta na gesi zaidi ya 30 ya mafuta nchini kwa lengo la kujadili changamoto walizonazo ili ziwasilishwe serikalini kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi.
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Godfrey Simbeye (aliyesimama)akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha makampuni makubwa ya wawekezaji sekta ya mafuta na gesi zaidi ya 30 kujadili changamoto walizonazo ili ziwasilishwe serikalini kwa ajili yakutafutiwa ufumbuzi. Mkutano huo umefanyika leo Aprili 4,2019 jijini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko, Blobu ya Jamii.

WAFANYABIASHARA wa kampuni kubwa za mafuta na gesi wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuendelea mchakato wa mradi wa kuchakata gesi na mafuta mkoani Mtwara kwa sababu hadi sasa hakuna kinachoendelea.

Pia wametaja changamoto nyingine inayokabili sekta hiyo ni kuhusu mikataba yao ya makubaliano ya uzalishaji na mauzo ya gesi na mafuta ambayo serikali iliichukua ili kuiangalia upya lakini hadi sasa haijairudisha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Godfrey Simbeye, amebainisha hayo leo Aprili 4, 2019 jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano uliyokutanisha kampuni kubwa za uwekezaji wa mafuta na gesi zaidi ya 30 kujadili changamoto walizonazo ili ziwasilishwe serikalini kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi.

Simbeye amesema walikutana na wafanyabiashara hao na moja ya changamoto waliowaeleza ni kutoona dalili zozote za kuanza kwa mradi huo wa gesi mkoani Mtwara ambao wanaamini ukianza utawanufaisha watu wengi. 

Kuhusu mikataba alisema wafanyabiashara hao wameomba Serikali iwarejeshee kwa sababu muda mrefu umepita tangu iichukua kwa ajili ya kuikagua.

"Mikataba hii ilichukuliwa na Serikali ili ikaguliwe ila mpaka sasa ni muda mrefu bado hawajairudisha jambo ambalo linakwamisha baadhi ya shughuli wanazozifanya hivyo wafanyabiashara wanaiomba na kuhimiza serikali iwarejeshe mikataba hiyo.

TPSF ilikutana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na kutueleza kuwa hadi mwishoni mwa mwezi huu watakuwa wameshakamilisha zoezi la kupitia mikataba hiyo hivyo tunasubiri kuona Kama ahadi hii itakuwa ya kweli, " alisema.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi ya TPSF, balozi Abdulsamand Abdulrahim amesema wamewaita wadau hao ili waweze kuwapatia mrejesho wa kazi za miezi mitano zilizofanywa na bodi hiyo hasa zile za kukutana na Serikali ili kuwasilisha changamoto za wafanyabiashara ili kuweza kuisaidia sekta ya mafuta na gesi.

Amesema, walishakutana Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na aliyekuwa Waziri wa Madini Angela Kairuki kwa vipindi tofauti na pia wamefanya mkutano mkubwa na dialogue baina ya AG na bodi ya TPSF kuwawasilishia chagamoto zinazozikabili sekta binafsi na wafanyabiashara.

Amesema, miongoni mwa kero wanazokutana nazo ni namna ambavyo wafabyabiashara wanasumbuliwa na TRA katika ulipaji kodi na baadhi viongozi ambao wanakwenda kukaa na kuwasumbua wawekezaji wakati hawana mamlaka ya kufanya hivyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: