AYUBU 14 :1-2
Mwanadamu aliye zaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu yeye uchanua kama vile ua, kisha ukatwa, ukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.

Mpende uliye naye na muonyeshe mapenzi ya kweli kwani kuna siku ataondoka utatafuta wa kumuonyesha mapenzi ya kweli hutampata.

Si kila mtu anafaa kuwa mke au kuwa mume, wewe uliye na mke au mume wako sasa huwezi elewe kwa haraka ila mjane aliyepoteza mume au mgane aliye poteza mke anaelewa nyakati anazopitia. Anatamani amuamshe mwenzake amuonyeshe upendo ila ndiyo haiwezekani tena.

Kuna Siri kubwa mbele za Mungu ya kuishi wawili na ndio sehemu ya kumalizia maisha yako ukiwa duniani maana ulisha zaliwa, ukakua ukatengana na wazazi sasa penye maisha ya mwisho kabla ya kuitwa na Mungu ni NDOA ndiYo mana andiko LINASEMA.

WAEFESO 5 :31-33
Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyo ni kubwa ila mimi na nena habari ya kristo na kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe wala mke asikose kumstahi mumewe.

Watu wengi wanachezea upendo wanaopewa leo na wake zao au waume zao kwa kuwa wanadhani hautakoma, siku ukikoma utajutaa. Kuna siku utatamani kumwambia mume wako au mke wako unampenda lakini hatakuwepo.

MPAMBE MWENZIO KWA MAUA KWA SASA AKIWA HAI AKIONA KWA MACHO YAKE MAUA YAKO, NI UPENDO. USINGOJE KUPAMBA KABURI LAKE KWA MAUA HAITASAIDIA TENA.

KWA NINI UTUMIE MUDA WAKO MWINGI KUTENGENEZA UGOMVI, CHUKI, NA MANYANYASO KWA MKEO AU MUMEO?

TAFAKARI MRUDIE MKEO AU MUMEO KWA MLIOACHANA, NA MLIO NDANI YA NDOA RUDISHENI AMANI, MUNGU ANASEMA NA NYIE WANANDOA KUPITIA UJUMBE HUU.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: