amanda wa Jeshi la Polisi nchini Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akizungumza na wakazi wa Dar es Salaam wakati wa uzinduzi ya wiki ya nenda kwa usalama mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika Viwanja vya Simu 2000
 Mwenyekiti wa kamati ya Usalama Barabarani, Big Boni akizungumza na wakazi wa Dar es Salaam kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama.
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabara kanda Maalum ya Dar es Salaam, Marison Mwakyoma akitoa taharifa fupi ya hali ya usalama barabara kwa kanda Maalum ya Dar es Salaam.
 Katibu wa Kundi la Uzalendo kwanza na Msanii wa Maigizo Kulwa Kikumba maharufu kama Dude akitoa neno la shukrani kwa kamanda wa kanda Maalum.
 Msaniii wa Muziki wa bongo fleva stara Thomas akitoa Burudani kwa kundi la wana Dar es Salaam waliofika hapo
 Wasanii wa Kundi la UZALENDO KWANZA Wakitoa burudani kwa wkazi wa Dar es Salaam.
 amanda wa Jeshi la Polisi nchini Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akisalimana na wasanii wa kundi la uzalendo kwanza

 amanda wa Jeshi la Polisi nchini Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akisikiliza maelezo kutoka kwa mkaguzi wa kituo cha Ubungo , Inspekta Ibrahim Samwix.
 Big Boni na Mwenyekiti wa Uzalendo kwanza, Steve Nyerere wakifuraia jambo mara baada yakumalizika kwa shughuli
Baadhi ya askari walishiriki uzinduzi wiki ya nenda kwa usalama.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Kamanda wa Jeshi la Polisi nchini Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa  amekipongeza kikundi cha Wasanii cha Uzalendo kwanza na kuahidi kushirikiana nao katika kampeni mbalimbali za kutokomeza ualifu na usalama barabrani.

Kamishana Mambosasa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua wiki ya nenda kwa usalama katika kanda maalum ambapo jeshi hilo kitengo cha usalama barabarani kilimualika kama kuw amgeni rasmi.

"Dar es Salaam kanda Maalum ndio sehemu pekeee ambayo ina askari wengi Tanzania nzima hivyo Wasanii waliopo Dar es Salaam na wingi wao ni lazima ufanane na uimara wa jeshi letu kama tunavyoona hapa mlivyojitolea katika kufanya kampeni hii ya usalama barabarani bila ya kujali umaharufu wenu mlionao katika jamii"amesema Mambo sasa.

aidha afande mambo sasa alisisitiza kuchukizwa na vitendo vinavyofanywa na kampuni za udalali za Tambaza na Excel kwa ukamataji wao katikati ya jiji bila kutumia weledi na kanuni za ukamataji salama.

amesema kuwa wafanyakazi wa kampuni hizo wamekuwa wakitumia nguvu hadi kufikia hatua ya kuwachapa madereva au abiria na bakora walizonazo hali inayosababisha madereva wengi kupata ajali .

kwa uapande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabrani kanda Maalum ya Dar es Salaam Big Boni amesema kamati yake itaendelea kushirikiana na jeshi la Polis kuakikisha ajali katika mkoa wa Dar es Salaam zinaisha kama sio kupungua kabisa.

Big Boni amesema kamati yake imejipanga kuakikisha inatoa semina kwa askari wa usalama barabrani , madereva bodaboda na vifaa vya kisasa kwa jeshi la polisi ikiwemo pikipiki na magari hili kufanya utendaji wao wa kazi kwa weledi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: