Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na watumishi wa Pori la Akiba la Swagaswaga mara baada ya kutembelea michoro ya mapangoni iliyochorwa zaidi ya miaka 1000 na kabila la Wasandawe katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ( wa pili kulia) akioneshwa michoro ya mapangoni na Askari Wanyamapori iliyochorwa zaidi ya miaka 1000 iliyopita na kabila la Wasandawe ambayo ni miongoni mwa vivutio vya Utalii wakati alipotembelea mara baada ya kuzungumza na watumishi wa Pori la Akiba la Swagswaga katika ziara yake ya kikazi wilayani Chemba jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Naibu Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi.
 Baadhi ya mawe makubwa ambayo yapo ndani ya Pori la Akiba la Swagaswaga ambayo yamechorwa michoro inayofafana na michoro inayopatikana Afrika Kusni.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (wa tatu kulia) akiangalia baadhi michoro ya mapangoni iliyochorwa zaidi ya miaka 1000 iliyopita na kabila la Wasandawe ambayo ni miongoni mwa vivutio vya Utalii wakati alipotembelea mara baada ya kuzungumza na watumishi wa Pori la Akiba la Swagswaga katika ziara yake ya kikazi wilayani Chemba jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Pori hilo, Alex Choya.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (wa tatu ) akitoka kuangalia baadhi michoro ya mapangoni iliyochorwa zaidi ya miaka 1000 iliyopita na kabila la Wasandawe ambayo ni miongoni mwa vivutio vya Utalii katika ziara yake ya kikazi wilayani Chemba jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Pori hilo, Alex Choya. (Picha zote na Wizara ya Maliasili na Utalii).

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewataka wananchi wafuate sheria kwa kujiepusha kuendesha shughuli za kibinadamu ndani ya Hifadhi ili kujenga mahusiano mazuri baina yao na Wahifadhi.

Pia, amewataka wananchi kuwachukulia Wahifadhi hao kama rafiki wa umma na watendaji waliotumwa na Serikali kulinda Maliasili kwa niaba yao.

Akizungumza na Watumishi wa Pori la Akiba la Swagaswaga katika wilaya ya Chemba jijini Dodoma, Mhe. Kanyasu amesema Wahifadhi wamepewa jukumu la kulinda hifadhi za Taifa na wamekuwa wakifanya kazi nzuri ya kuifanya Tanzania iendelee kuwa na maeneo mazuri yaliyohifadhiwa.

''Sisi ni wa moja hakuna haja ya kujengeana uhasama kati yetu, Wananchi wafuate sheria za Uhifadhi na Wahifadhi fuateni sheria wakati mnapokabaliana na Wananchi'' amesisitiza Kanyasu.

Amesema Wahifadhi wa Wanyamapori na Misitu wanazilinda rasilimali hizo kwa ajili wote, vitu kama mvua, hali ya hewa safi pamoja na mvua ni moja ya faida za moja kwa moja zinazopatikana kutokana na maeneo yaliyohifadhiwa vizuri.

Amesema Wahifadhi hao wameajiriwa kwa mujibu wa sheria hivyo hutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya kazi zao na pale wanapokiuka sheria mamlaka zinazohusika huwachukulia hatua.

“Sisi kama Wizara tunaamini kwamba wahifadhi wetu wanafanya kazi nzuri, pale ambapo wamekuwa wakilaumiwa kwa kuwapiga na kuwanyanyasa watu kwa namna yoyote ile tumetuma Tume maalum kuchunguza na kuchukua hatua” Amesema

Mhe, Kanyasu amesema uchunguzi unapofanyika na ikathibitika kuwa tukio lililofanyika halikuongozwa na matumizi ya sheria na kuwepo kwa haki wizara imekua ikichukua hatua.

Ameeeleza kuwa Wahifadhi ni watu muhimu saba kwa vile bila wao hakuna uhifadhi unaoweza kuendelea nchini akibainisha kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakipinga juhudi za uhifadhi kwa kuwatetea watu wanaovunja sheria.

Kuna watu wanatamani kuona misitu na wanyamapori wote tunawamaliza ili wapate maeneo ya malisho na kilimo, Nawambieni tukithubutu kufanya hivyo huu ndo utakuwa mwisho wetu wa maisha" Amesisitiza Mhe.Kanyasu

Amesema yapo madhara makubwa yanayoweza kutokea kama hakutakuwa na uhifadhi imara ikiwemo maeneo mengi ya nchi kugeuka kuwa jangwa kutokana na uharibifu wa misitu, ukosefu wa mvua, ukosefu wa maji, chakula na ukosefu wa hewa safi.

Kwa upande wake, Meneja wa Pori la Akiba la Swagaswaga, Alex Choya amesema kuwa kumekuwa na tuhuma za vitendo vya ukatili dhidi ya raia vinavyofanywa na baadhi ya askari wa hifadhi za Taifa na kutoa wito kwa wananchi wote wenye ushahidi na taarifa juu ya vitendo hivyo kuziwasilisha ili hatua stahiki zichukuliwe.

Amesisitiza kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) hairuhusu askari kufanya vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya raia badala yake imekua ikiwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa rasilimali zinazowazunguka.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: