Daktari bingwa wa watoto wachanga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Augustine Massawe akizungumza wakati akitoa mafunzo ya Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) kwa wafanyakazi wa hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es salaam lengo likiwa ni kuwapatia uelewa wafanyakazi walioko katika makampuni na taasisi mbali mbali nchini. Mafunzo hayo yaliratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel na itakuwa ni programu inayoendelea kufikisha ujumbe kwa jamii nzima kujua mambo mengi kuhusu watoto njiti na namna ya kujitahidi kuzuia kuzaliwa kwa watoto kabla ya muda wao.
Sehemu ya Wafanya kazi wa hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es salaam wakifatilia mafunzo hayo yaliyokuwa yakitolewa na Daktari bingwa wa watoto wachanga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Augustine Massawe ambaye pia ni Balozi wa Watoto Njiti nchini.
Meneja wa Mafunzo wa hoteli ya Hyatt Regency, Prince Robert akizungumza jambo wakati wa mafunzo yaho yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: