Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) wakati Mkuu wa mkoa huyo alipokuwa akipokea nyaraka mbalimbali toka kwa viongozi wa Yanga ili kukamilisha ununuzi wa kiwanja cha klabu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Bw. Omar Kaya.
Baadhi ya viongozi wa klabu ya Yanga wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (hayupo pichani) wakati Mkuu wa mkoa huyo alipokuwa akipokea nyaraka mbalimbali toka kwa viongozi hao ili kukamilisha ununuzi wa kiwanja cha klabu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) akipokea baadhi ya nyaraka toka Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dkt. Mshindo Msolla ili kukamilisha ununuzi wa kiwanja cha klabu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, wanaoshuhudia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) na Kaimu Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Bw. Omar Kaya.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwapongeza viongozi wa klabu ya Yanga (hawapo pichani) kwa hatua waliyofikia katika ununuzi wa uwanja, kulia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Bw. Omar Kaya.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: