Mbunge wa Starehe, Charles Njagua maarufu Jaguar amekamatwa na polisi nchini Kenya akiwa eneo la jengo la Bunge kwa madai ya kutoa vitisho dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni.

Jaguar ambaye bado anashikiliwa na polisi amekamatwa leo jumatano katika viwanja vya bunge na hiyo ni baada ya kushindwa kuripoti katika kituo cha polisi kama alivyoagizwa .

Serikali nchini Kenya imejiweka kando na kauli hiyo ya Jaguar ambayo ilipinga kufanya biashara na na wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nchi za nje.

Taarifa iliyotolewa na mamlaka ilikemea Uhuru wa kuongea uluotumiwa na mbunge huyo katika kudhalilisha wawekezaji kitu ambacho si utamaduni wa nchi hiyo na unapaswa kukemewa.

Kupitia video iliyosambaa kupitia mitandao ya kijamii Jaguar alionekana akikemea uwepo wa wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nje na kueleza kuwa wataondolewa kwa nguvu wasipotii agizo Hilo.

Lakini Waziri wa mambo ya nje Macharia Kamau amesema kuwa Kenya imesikitishwa Sana na kauli ya Mbunge huyo hukuakieleza kuwa serikali ya Kenya haikubaliani na kauli hiyo na amewahakikishia usalama kwa wawekezaji wote nchini humo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. Hongera sana Hii blog ni nzuri sana naitembelea kila saa kupata vitu vipya, Hii ni blog pekee iliyobaki Tanzania, Pia nilitaka kuwajulisha watanzania wenzangu kuwa kuna mtandao unalipa kwa kupost mambo ya kielimu bonyeza jina langu hapo kushoto kwenye komenti hii ujifunze zaidi. sasa mitandao ya kijamii inalipa

    ReplyDelete