Na Mwandishi wetu Mihambwe

Mwenyekiti wa Kijiji cha Namunda kilichopo kata ya Kitama kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) Suleiman Mkubulu amerejesha mifuko 24 aliyoitumia kinyume na utaratibu kama alivyohaidi kuirudisha baada ya Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu kugundua upotevu wa mifuko hiyo alipokuwa akifuatilia kwa makini ujenzi wa miradi ya maendeleo kijijini hapo.

Tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na Afisa Tarafa Mihambwe, Diwani kata ya Kitama, Mtendaji kata Kitama, Mtendaji Kijiji Namunda, Wajumbe Serikali ya Kijiji pamoja na kamati ya ujenzi.

Akizungumza mara baada ya mifuko hiyo kukabidhiwa kimaandishi kwa Mtendaji wa Kijiji na kamati ya ujenzi, Gavana Shilatu aliwasihi sana viongozi kuelewa dhana ya utumishi na uongozi ni dhamana ya Wananchi na si mwanya wa kujitajirisha, kudhulumu au kuonea wengine kinyume na sheria.

"Pasipo usimamizi imara, hii mifuko 24 ya saruji ingepotea. Ni lazima tutambue uongozi ni dhamana na si fursa ya kujitajirisha au kuonea wengine."* Alisema Gavana Shilatu

Tangu awali alipopata taarifa ya upotevu, Gavana Shilatu alisimama kidete hadi saruji hiyo kurejeshwa kwa ajili ujenzi wa miradi ya maendeleo ya ofisi ya Kijiji na Madarasa mawili na ofisi moja ya Walimu ya Shule ya msingi Namunda.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: