Meza kuu watatu kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambaye ni mgeni wa heshima na Mkuu wa Nchi pekee kutoka Bara la Afrika akiwa katika mkutano wa waratibu wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika. Wa pili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje China na Mjumbe wa Baraza la Taifa Mhe. Wang Yi. Mkutano huo umefanyika Beijing,China na Kuhudhuriwa na Mawaziri wa mambo ya Nje wa Nchi za Afrika 53. June 25, 2019.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba John Kabudi (Mb) (katikati) akifuatilia mkutano wa waratibu wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC),Beijing - China. June 25, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) (watano kutoka kushoto) akiwa katika mkutano wa waratibu wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaohudhuriwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje 53 kutoka Nchi za Afrika. Mkutano huo unafanyika Beijing – China. June 25, 2019.
Sehemu ya Mawaziri wa mambo ya Nje kutoka Nchi 53 za Afrika wanaohudhuria mkutano wa waratibu wa jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).Mkutano huo unafanyika Beijing – China. June 25, 2019. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: