Je, una marafiki wanao kuhamasisha kufikia ndoto zako? Je, unao marafiki wanaosaidia kuyafikia matarajio yako? Je, unao marafiki wanaotamani kuona unafanikiwa maishani?

Kama unao watu/marafiki wa namna hiyo basi jihesabu kuwa miongoni mwa watu wenye bahati kubwa duniani! Marafiki wa kweli hukuhamasisha na kukutia moyo ili uweze kufanya mambo makubwa kwa ajili yako na kwa ajili ya wengine!

Msomi John Mason kupitia kitabu chake cha The impossible is possible aliandika andiko kuwa Your best frien ds are those who bring out the best in you! Huyo ndiye rafiki wa kweli, anayependa kuona unafanikiwa! Anayependa kuona unafikia malengo yako! Anayekuhamasisha kutimiza ndoto zako! Huyo ndiye rafiki wa kweli!

Tusipende kutumia muda mrefu kuishi na marafiki wanafiki wanaokuwa na ngozi ya kondoo tukiwa nao kumbe ni mbwa mwitu wakali wakiwa mbali nasi! Watu wasiopenda kuona tunapiga hatua! Watu waliotayari kuona tunashindwa, tunateketea na kudidimia! Hawa siyo marafiki! Ni maadui zetu!

Msomi huyu huyu John Mason kupitia kitabu chake hicho hicho cha The impossible is possible aliandika kuwa He that walks with wise men shall be wise, but a companion of fools shall be destroyed!! Ndiyo! Hata wahenga walisema kuwa "ukikaa karibu na Waridi lazime unukie!" Kwahiyo ukitembea na watu wenye hekima utakuwa na hekima ila ukiendelea kuishi na wanafiki na wapumbavu utaangamia!!!

Tatizo ni kwamba tutawapataje marafiki hawa wa kweli? Tutawezaje kuwatofautisha marafiki wa kweli na wanafiki?

Tutaweza kuwatambua watu wa aina hii kutokana na maisha tunayoishi! Kazi tunazozifanya na watu wanaotuzunguka!

Haiwezekani tukatarajia kuzungukwa au kuwapata marafiki wa kweli wakati sisi tabia na mienendo yetu haiendani nao! Kama sisi tuna mawazo hasi sawa na wanafiki hatuwezi kuwa na marafiki wa kweli! Lazima tuamue kuwa wa moto au wa baridi siyo wa uvuguvugu tukiwa wa uvuguvugu hatutaeleweka! wa moto/chanya ni watu waadarifu, wanaowaza maendeleo, wanaowaza kusonga mbele, wanaowaza kufanikiwa wao na watu wengine wanaowazunguka lakini hawa wa baridi/hasi huwaza kutofanikiwa, huwaza kuwasengenya wengine, kufurahia kushindwa kwa wengine, wasiowaza kuhusu kesho yao wala yako! Hawa ndio hawafai kabisa! Na hawa wa uvuguvugu huwaza unafiki, kupika majungu, kusema uongo kwa maslahi ya matumbo yao! Hawa ni viwavi! Hawa huiharibu jamii! Hawa hufarakanisha! Hutengeneza chuki kwenye jamii! HAWAFAI KABISA!!

Tukumbuke siku zote rafiki mwema na wakweli hawezi kufuata njia usizofuata! Yeye huwa tayari kuungana na wewe kama anaona tayari una wema ndani yako na atakuwa na wewe wakati wa jua lakini pia wakati wa mvua! Ukiona yupo rafiki anakuwa na wewe wakati wa mvua tu na likifika jua anakukimbia achana naye ni mnafiki huyo!

TUJITAFAKARI KWA MASLAHI MAPANA YA MAENDELEO YETU!

Mh. Bonnah L. Kamoli (MB)

Jimbo la Segerea, Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: