UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeuandikia barua Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) sambamba na Shirikisho la soka Nchini (TFF) kujiondoa kwenye michuano ya Kagame inayoatarajiwa kuanza mapema mwezi ujao nchini Rwanda.

Mapema wiki iliyopita, CECAFA waliwaandikia barua Yanga ya kuwaalika kwenye michuano hiyo ambapo uongozi wa Yanga ulikuwa unasubiri kauli ya Kocha Mkuu ws timu hiyo Zahera Mwinyi kama watashiriki au la.

Yanga wameandika barua hiyo wakielezea sababu mbalimbali za kujiondoa kwao kwenye michuano hiyo ikiwemo kumalizika kwa mikataba kwa wachezaji wao wengi.

Awali Uongozi wa Klabu ya Simba ulishafanya maamuzi na kuamua kujiondoa kwenye michuano hiyo ila kwa upande wa mabingwa watetezi wa kombe hilo Azam wao wamethibitisha kushiriki.

Michuano ya Kagame inatarajiwa kuanza Julai nchini Rwanda ikishirikisha timu mbalimbali kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: