Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia Bi. Grace Mwangwa akifungua zoezi la majalibio ya Kitini cha Mafunzo ya masuala ya ukatili wa kijinsia yanayoendelea leo Mjini Morogoro.
Baadhi ya Wadau wa masuala ya Jinsia wakijadiliana wakati wa zoezi la majalibio ya Kitini cha Mafunzo ya masuala ya ukatili wa kijinsia yanayoendelea leo Mjini Morogoro.
Baadhi ya Wadau wa masuala ya Jinsia wakijadiliana wakati wa zoezi la majalibio ya Kitini cha Mafunzo ya masuala ya ukatili wa kijinsia yanayoendelea leo Mjini Morogoro.

Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleao ya Jamii inakutana na wadau mjini Morogoro kufanya majaribio ya kitini kilichoandaliwa na Wizara hiyo kwa lengo la kuimarisha uwezo wa wawezeshaji kupata maarifa na stadi juu ya mikakati ya kijamii ya kuzuia ukatili wa kijinsia hapa Nchini.

Akiongea na wadau mbalimbali Mkoani humo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Grace Mwangwa amesema kuwa kitini hicho kina mada mbalimbali zitakazowezesha kutoa mwongozo wa kitaifa wa mafunzo ya kijinsia yatakayowawezesha walengwa kubainisha na kukemea mila na desturi zenye kuleta madhara kwa jamii ikiwemo mafunzo kuhusu kuzingatia masuala haki za kijinsia.

Bi. Mwangwa amesema kwamba kuwepo kwa Kitini hicho pia kutasaidia katika kupunguza au kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia na hivyo kuwawezesha wanafamilia hususani wanawake kushiriki katika shughuli za kiuchumi. 

Bi. Mwangwa ameongeza kuwa utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria ya mwaka 2015-2016 unaonesha kuwa wanawake 4 kati ya 10 wamefanyiwa ukatili wa kimwili wakiwa na umri wa miaka 15 akiongeza kuwa Ukatili wa kimwili unaongezeka kadri umri unavyoongezeka.

Pamoja na idadi kubwa ya wanawake kufanyiwa ukataili wa kimwili Bi. Mwanga pia amesema 22% ya wanawake wenye umri wa miaka 15-19 wamefanyiwa ukatili wa kimwili, ukilinganisha na asilimia 48 ya wanawake wenye umri wa miaka 40-49 na kuongeza kuwa takwimu za hali ya Uhalifu na Usalama barabarani zinaonesha pia kwa kipindi cha Januari- Desemba 2016 mpaka Januari – Desemba 2016 zinaonesha kuwa jumla ya wanawake 307 walipata ukatili wa kimwili ukilinganisha na takwimu za kipindi cha Januari - Disemba 2017 ambapo jumla ya wanawake 350 ambao walipata ukatili wa kimwili.

Aidha Bi. Mwangwa amewaambia wajumbe wa kikao kazi hicho kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imedhamiria kushughulikia ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa kuweka sera, sheria na mipango inayolenga kulinda haki za wanawake, watoto na makundi mengine ya kijinsia. 

Amezitaja juhudi za Serikali katika kupambana na ukatili wa kijinsia kuwa ni pamoja na kuridhia mikataba za kimataifa na Kikanda yenye lengo la kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuleta usawa wa kijinsia lakini pia kutunga sheria mbalimbali zenye mlengo wa kulinda na kuendeleza haki za binadamu.

Bi. Mwangwa amezitaja sheria hizo kuwa ni pamoja na za sheria ya Mtoto (2009), Sheria ya watu wenye ulemavu, UKIMWI, makosa ya Jinai, ajira, ardhi, msaada wa kisheria, usafirishaji haramu wa binadamu, ndoa, mirathi, elimu, na uwezeshaji kiuchumi.

Maandalizi ya Kitini hiki ni moja ya hatua muhimu ya utekelezaji wa mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa miaka mitano ambao uliandaliwa mahususi kupambana na kutokomeza vitendo vyote vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: