Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na wanahabari ndani ya Maonesho ya 43 ya Kitaifa ya Biashara Sabasaba 2019 mara baada ya kutembelea banda lao kungalia jinsi wanavyotoa huduma kwa wananchi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (kwanza kushoto) akisikiliza watoa huduma mara baada ya kuwasili bandano hapo kujionea jinsi wanavyotoa huduma.

 Dawati la huduma kwa wateja wakiendelea kutoa huduma kwa wateja waliofika kwenye Banda la Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) kwenye Banda lao la Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akifafanuliwa jambo na dawati la kutoa huduma kwa wananchi.
Mwanahabari Zaynab akipata maelezo ya vifaa vinavyotumika katika kuungalishia wateja maji.

Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) akipata maeleozo kutoka kwa Meneja Uhusiano wa DAWASA Joseph Mkonyi (kushoto) mara baada ya kutoka katika banda lao lililopo katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba 2019.

Zainab Nyamka na Cathbert Kajuna, Globu ya Jamii


Afisa Mtendaji Mkuu wa Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja ameweka wazi kuwa tatizo la maji ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani linaenda kuisha.

Luhemeja ameyasema hayo alipotembelea banda la DAWASA lilipo ndani ya maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari baada ya kupata maelezo kutoka kwa watoa huduma kwa wateja na wahandisi, Luhemeja amesema shida ya maji ndani ya mkoa wa Dar es Salaam na Pwani inaelekea kuisha kutokana na miradi mbalimbali inayoendelea kujengwa na ile mipya.

Luhemeja amesema, wameshasaini miradi mikubwa sita ya maji yenye thamani ya bilion 114.5 ambapo itasambaza maji ndani ya mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

"Wananchi walikua na shida ya maji na miradi hii mikubwa inaenda kuondoa changamoto ya maji  na malengo kufikia asilimia 95 mwaka 2020," amesema Luhemeja.

Amesema, kwa sasa maji yanapatikana kwa asilimia 85 tofauti na miaka ya nyuma ambapo maji yalikua asilimia 68 na mapato yamepanda kutoka bilion 3.2 kwa mwezi hadi bilioni 11.2.

Akielezea sheria mpya namba 5 ya mwaka 2019 inayoibadilisha mamlaka ya majisafi na majitaka na kuwa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira, Luhemeja amesema wameipokea vizuri na itasaidia katika kulinda vyanzo vya maji  na kudhibiti usafi wa mazingira.

Aidha, Luhemeja amesema DAWASA bado wanaendelea na kusajili wamiliki wa Visima na kuhakiki ubora wa maji na kuwajua kutokana na sheria mpya kuwaondolea kodi ya kila mwaka.

Ametoa rai kwa wananchi kufika kwenye banda lao lilipo ndani ya maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam ili kufahamu miradi ya maji inayoendelea kujengwa na mipya itakayoondoa changamoto ya maji ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: