Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (watatu kushoto), akizungumza jambo mbele ya Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter (katikati) na Mussa Mwambujule, Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko, wakati alipotembelea banda la WCF kwenye maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi Simiyu. 
Afisa Uhusiano Mwandamizi WCF, Bw. Sebera Fulgence (kulia) akitoa elimu ya Fidia kwa wafanyakazi.
Mussa Mwambujule, Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), akitoa elimu hiyo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, akisalimiana na mama huyu aliyefika banda la WCF kupata elimu ya Fidia kwa wafanyakazi
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu.

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), hivi karibuni uko mbioni, kuanzisha mfumo wa waajiri na wafanyakazi kuwasilisha madai ya Fidia kwa njia ya mtandao, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo Bw. Anselim Peter ameyasema hayo jana kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Bw.Peter alisema lengo la kuanzisha mfumo huo ni kusogeza karibu huduma za Mfuko kwa wateja wadau wake na hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi unashiriki katika maonesho ya Nanenane kwa lengo la kupata fursa ya kuwaelimisha waajiri na wafanyakazi kuhusu shughuli za Mfuko ambazo ni kulipa Fidia, utaratibu gani wa kufuata ili kuwasilisha madai kabla ya kulipwa Fidia.

"Pia katika banda la WCF hapa Nyakabindi, wataalamu wetu watatoa elimu kuhusu Mfuko, kusajiliwa, kuwafahamisha taratibu za michango, kuwafahamisha taratibu za madai ya fidia na pia kupokea maoni ya wadau kuhusu Mfuko. Lakini pia tunatoa huduma kwa vitendo jinsi wanavyoweza kufanya kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wafanyakazi wake kwenye orodha iliyoko WCF, kuprinti cheti, na pia kulipa michango ofisini kwako.” Alifafanua Bw. Peter.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mtaka, ameupongeza Mfuko huo kutokana na ushiriki wake katika mpango wa Mkoa kujenga kiwanda cha kutengenza vifaa tiba Huu ni utekelezaji kwa vitendo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuanzisha na kuimarisha viwanda ambavyo vitaipeleka nchi kafika uchumi wa Kati.

"Nishukuru na kutambua mchango mkubwa wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba na WCF kwa ujumla kwa sababu ni partner (Mshirika) Mkubwa kwenye mipango yetu ya ujenzi wa kiwanda cha Vifaa tiba." Alisema Mhe. Mtaka.

Alisema uongozi wa Mkoa walishirikiana na WCF katika hatua mbalimbali za kushirikiana katika ujenzi wa kiwanda hicho ambapo tayari site clearance imeshafanyika na kwamba hivi sasa wizara iko katika nafasi nzuri ya kutangaza zabuni ili kumpata mkandarasi atakayejenga kiwanda hicho.

"Kwetu sisi kama mkoa WCF imetoa ushirikiano mkubwa katika mipango yetu ya kushiriki katika uchumi wa viwanda wametoa ushirikiano mkubwa." Alisema Mkuu wa Mkoa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: