Mkurugenzi wa Huduma za Airtel Money Isaack Nchunda akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati kampuni ya Airtel Tanzania ikitangaza kugawa faida ya jumla ya Tsh2.5 bilioni kwa wateja na mawakala wake wote wanaotumia huduma ya Airtel Money baada ya kupata kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Airtel imekuwa ikizirudisha kwa wateja wake waliotumia Airtel Money kwa kila robo ya mwaka kulingana na kiwango ambacho kipo kwenye akaunti zao za Airtel Money kila siku. Kulia ni Meneja Uhusiano Airtel Jackson Mmbando.
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati kampuni ya Airtel Tanzania ikitangaza kugawa faida ya jumla ya Tsh2.5 bilioni kwa wateja na mawakala wake wote wanaotumia huduma ya Airtel Money baada ya kupata kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania(BOT). Airtel imekuwa ikizirudisha kwa wateja wake waliotumia Airtel Money kwa kila robo ya mwaka kulingana na kiwango ambacho kipo kwenye akaunti zao za Airtel Money kila siku. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Airtel Money Isaack Nchunda.
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora za kidigitali ,imetangaza kugawa faida ya jumla ya Tsh2.5 bilioni kwa wateja na mawakala wake wote wanaotumia huduma ya Airtel Money baada ya kupata kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania(BOT)

Faida itokanayo na Airtel Money ni fedha ambayo Airtel imekuwa ikizirudisha kwa wateja wake waliotumia Airtel Money kwa kila robo ya mwaka kulingana na kiwango ambacho kipo kwenye akaunti zao za Airtel Money kila siku. Kiwango hicho cha faida kwa kila salio la mteja kinatolewa pia kulingana na jinsi mteja anavyotumia huduma ya Airtel Money, mteja atatumiwa faida yake kwenye akaunti yake ya Airtel Money na anaweza kuamua kuzitoa,kutuma au kuzitumia kwa matumizi yoyote ikiwemo kulipia bili mbalimbali kama vile za DAWASCO, LUKU, MALIPO YA SERIKALI na mengine mengi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kugawa faida hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda alisema “faida itokanayo na matumizi ya Airtel Money itagawiwa kwa wateja wa Airtel Money na mawakala wote nchini ambao wametumia huduma ya Airtel Money kwa miezi kumi na mbili iliyopita kati ya September 2018 hadi March 2019.

“Airtel inaendelea kuunga mkono juhudi za serikali zanazochochea kusambaa na upatikanaji wa huduma za kifedha hapa nchini kwa kutoa faida kila robo ya mwaka, faida hii itawawezesha wateja kupata jumla ya Tzs2.5bn zitakazokwenda kwa wateja na mawakala waliotumia huduma kwa kipindi hicho. Tunayo furaha kuona ukuaji mzuri kwenye huduma ya Airtel Money kwani mpaka sasa huduma zetu zimekuwa zikikuwa mfululizo kwa ukuaji wa tarakimu mbili, alisema Nchunda.

Nchunda aliongeza kuwa hii ni mara ya nane Airtel inatoa faida kwa wateja wake wote wa Airtel Money tangu mwaka 2015. Mpaka sasa jumla ya kiasi cha Tsh19 bilioni kimeweza kutolewa kama faida kwa wateja na mawakala wote nchini.

“Kuanzia leo wateja wote wa Airtel Money wataweza kutumia fedha zao za faida kwa kununua LUKU, kununua muda wa maongezi au bando au kwa matumizi yeyote yale”. Alisema Nchunda

Airtel Tanzania imedhamiria kuendelea kuboresha na kuleta karibu huduma za Airtel Money ili kufikia maelfu ya Watanzania ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki na hasa kwa maeneo ya vijijini. Kwa kufanikisha hilo, hivi karibuni Airtel ilizindua kampeni ya Tuko Nawe Kila Kona kwa lengo la kuimarisha huduma ya maduka ya Airtel Money Branches ambayo ni moja kati ya mikakati muhimu ya kusambaza huduma ya Airtel Money hapa nchini. Vilevile Airtel imezindua bando za Dabo Data Smatika kupitia Airtel Money kwa lengo la kuongeza huduma kwenye huduma zinazotolewa na Airtel Money branches zaidi ya 1000 nchini

Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano wa Airtel Jackson Mmbando alisema kuwa “Lengo letu ni kuendelea kuwafikia wateja wetu ambao ni muhimu sana kwenye biashara yetu. Tunaendelea na uzinduzi wa maduka ya Airtel Money Branches ili kuhakikisha kuwa na huduma za kifedha za Airtel Money zinaendea kupanuka na kuwafikia wateja wengi kuliko huduma yoyote ya kifedha nchini . Wateja wetu tunawahakikishia huduma ya papo kwa hapo za kutoa pesa ni BURE.

Airtel bado itaendelea kuhakikisha ya kwamba inapanua wigo wa mawakala kwa ajili ya kufikisha huduma za kifedha kupitia simu za mkononi kwa Watanzania wote mjini na vijinini.

Mmbando alimalizia kwa kusema kuwa “Ili kuendana na kasi ya ukuaji wa huduma ya Airtel Money pia tumejiunga na huduma zingine zenye tija kwa watumiaji kama vile e-government ambapo wateja wanaweza kufanya malipo ya huduma mbali mbali kama vile malipo ya tozo za ardhi, kodi za serikali, kwa wakati mmoja. Pia huduma ya Airtel Money imeunganisha zaidi ya benki 40 ili kuwawezesha wateja kuhamisha fedha kutoka akaunti ya simu za mkononi kwenda benki na vile vile kutoa benki kuweka kwenye akaunti za simu za mkononi wakati wowote”.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: