Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akikagua ujenzi wa darasa katika Shule ya Msingi Italala Kata ya Sepuka mkoani Singida alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi na kujitambulisha kwa wananchi baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli kuongoza wilaya hiyo.
 DC Mpogolo akiangalia eneo la kulowanisha ngozi wakati alipokuwa akikagua Kiwanda Kidogo cha Kusindika Ngozi katika Kijiji cha Msungua.
 DC Mpogolo akikagua mashine ya kutotolesha vifaranga na mayai iliyopo Kijiji cha Msungua ambayo haizalishi chochote.
 DC Mpogolo akikagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mnang'ana.
 DC Mpogolo akipata maelezo ya uchimbaji wa kisima cha maji katika Kijiji cha Mnang'ana.
 Hapa DC Mpogolo akiangalia jengo la Soko la Kata ya Sepuka ambalo ujenzi wake umesimama tangu mwaka 2013. Anaye toa maelezo ni Diwani wa Kata ya Sepuka Yusuf Misanga.
 Afisa Tarafa ya Sepuka, Corlinel Nyoni akiwatambulisha viongozi katika mkutano wa hadhara.
 Diwani wa Viti Maalumu wa Kata ya Sepuka, Halima Athumani akizungumza.
 Ulinzi ukiimarishwa katika mkutano wa hadhara.
 Diwani wa Kata ya Sepuka, Yusuf Misanga akizungumza.
 DC Mpogolo akihutubia.
 Mkazi w Kata hiyo Kitiku Memba akizungumzia kuhusu migogoro ya ardhi.
 Mzee Seleman Majilanga akizungumzia kudhurumiwa shamba lake.
 Mariam Muna akizungumzia kuhusu ardhi.
 Athumani Nkindu akizungumzia ujenzi wa shule.
 Mzee Iddi Mwango akizungumzia kuporwa shamba.
 Mkutano ukiendelea.
 Wazee wa Kata ya Sepuka wakiwa kwenye mkutano huo.
 DC Mpogolo akimkabidhi Lucas Lissu cheti baada ya kuhitimu mafunzo ya usaidizi wa kisheria.
Maria Kingu akikabidhiwa cheti cha usaidizi wa kisheria.

Na Dotto Mwaibale, Singida.

MABARAZA ya kata ya usuluhishi wa migogoro ya ardhi yametakiwa kutenda haki na kutojihusisha na vitendo vya rushwa.

Ombi hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,  Edward Mpogolo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Sepuka mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi na kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli kuongoza wilaya hiyo miezi miwili iliyopita.

" Nayaomba mabaraza yote ya kata ya usuluhishi migogoro ya ardhi yawatendee haki walalamikaji na kuacha kuchukua rushwa kwa walalamikiwa na kupindisha haki" alisema Mpogolo.

Mpogolo katika mkutano huo aliwageukia wasaidizi wa msaada wa  kisheria katika wilaya hiyo waliopata mafunzo kwa kuwezeshwa na Wizara ya Katiba na Sheria kufanya kazi hiyo kwa weredi bila ya kuwatoza wananchi fedha na kutoa hukumu.

Alisema kazi yao ni kuwapa msaada wa kisheria wananchi bure na sio kuhukumu na pale wanapoona mashauri yamekuwa magumu wanatakiwa kuyapeleka ngazi nyingine ya utatuzi.

Katika mkutano huo DC Mpogolo alibaini Kata ya Sepuka kuwa na migogoro mingi ya ardhi ukilinganisha na kata zingine huku ikiwahusisha ndugu na jamaa wa karibu.

Mzee Seleman Majilanga alimwambia DC Mpogolo kuwa mabaraza ya ardhi ya kata yamekuwa na changamoto katika kutatua migogoro kutokana na wajumbe kujihusisha na rushwa na kupindisha haki.

Katika ziara hiyo DC Mpogolo alikagua ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Italala, zahanati ya Mnang'ana, kiwanda kidogo cha kusindika ngozi kilichopo Kijiji cha Msungua na jengo la soko Kata ya Sepuka ambalo ujenzi wake ulisimama tangu mwaka 2013.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: