Baada ya Tanzania kuwa Mwenyekiti wa SADC, mikutano mbali mbali ya SADC itaendelea kufanyika nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi Agosti, 2019.

Kufuatia utaratibu huo , tarehe 16 hadi 20 Septemba, 2019 kutakuwa na Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa. Mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam.

Masuala mbali mbali yanayohusu Sekta hizo ikiwemo sera, mikakati, programu na miradi itajadiliwa na kikao cha awali cha Viongazi Waandamizi na mapendekezo yao kuwasilishwa kwenye kikao cha Waheshimiwa Mawaziri kwa ajili ya majadiliano na maazimio.

Tarehe 16 hadi 18 Septemba, 2019 kutakuwa na Mkutano wa Senior Officials ambao ni Makatibu Wakuu na Viongozi Waandamizi wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa.

Ambapo tarehe 19 Septemba, 2019 kutakuwa na mkutano wa High Level Roundtable Dialogue wa Mawaziri na wadau wengine wanaohusika, ikiwemo taasisi mbali mbali na sekta binafsi.

Aidha, tarehe 20 Septemba, 2019 kutakuwa na Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa.

Mkutano wa Makatibu Wakuu utafunguliwa na kufungwa na Waheshimiwa Mawaziri.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: