Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanaokutana kuanzia leo Septemba 16, 2019 jijini Dar es Salaam. Picha zote na Matokeo Chanya+.

Na Mwandishi Wetu.

NCHI za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), zipo katika mkakati wa kuwa Mfumo Satelaiti ambapo utawezesha taarifa za nchi hizo kudhibitiwa katika ukanda huo bila kuvuka mipaka.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe  wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa waliokutana jijini Dar es Salaam.

Waziri Kamwelwe ameema kwa muda mrefu nchi za SADC zimekuwa zikitumia mfumo wa Satelaiti ambao unahitaji taarifa kwenda katika nchi za Ulaya na Marekani ndio zirudi nchini na kumfikia muhusika hivyo wanataka kuondokana na utaratibu huo.

Amesema maofisa hao waandamizi watatumia mkutano huo kujadili na kuja na ubunifu ambao utarahisisha kila nchi mwanachama kusimamia mawasiliano yake bila kutegemea uthibiti kutoka nje ambao sio salama kwa nchi na watuamiaji.

“Mkutano huu huu wa siku tano wa sekta ya Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa ni mwanzo mzuri wa nchi za SADC kuweka mazimgira salama katika mfumo wa ke wa taarifa na mawasiliano ya inteneti kwani tupo kwenye mkakati wa ujenzi wa Satelaiti ya pamoja hivyo kuachana na mifumo ya zamani,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miundombinu SADC, Mapolao Mokoena amesema mkutano huo utaweza kusaidia uelewa wa watendaji wa Serikali kujua njia ya kupita katika kuifanya jumuiya ifikie malengo yake hasa katika miundombinu.

Mokoena alisema baadhi ya nchi zimeonesha uthubutu katika ujenzi wa miundombinu akitolea mfano wa Tanzania hivyo kuzitaka nchi zingine ziongeze jitihada katika eneo hilo ambalo ni muhimu katika kukuza uchumi wan chi husika.

“SADC ina program yake ya kuendelea miundombinu katika sekta zote hivyo mkutano huu ni mwanzo mzuri wa utekelezaji huo ni imani yangu kuwa tutaweza kufikia mazimio yenye tija kwa kila nchi mwanachama,” alisema.

Mkurugenzi huyo ambaye alimuwakilisha Katibu Mkuu wa SADC, Dk.Stergomena Tax alisema sekta ya Tehama, Bahari, Uchukuzi na Hali ya Hewa ni sekta muhimu katika kukuza uchumi hivyo ni vema kila nchi kuwekeza katika eneo hilo.
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi.
Mkurugenzi wa Miundombinu SADC, Mapolao Mokoena amesema mkutano huo utaweza kusaidia uelewa wa watendaji wa Serikali kujua njia ya kupita katika kuifanya jumuiya ifikie malengo yake hasa katika miundombinu.
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi.
Viongozi wakifuatilia kwa makini.
Meza kuu.
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe akicheza ngoma mara baada ya kumaliza kufungua mkutano.
Burudani ya Ngoma.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: