Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mjini Iringa akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo Septemba 25, 2019. Kushoto ni Mkugenzi Mtendaji wa Makampni ya ASAS na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wa Mkoa wa Iringa, Salim Abri na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Fuad Abri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kulia) wakitazama maziwa yaliyofungashwa wakati walipotembelea kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mjni Iringa, Septemba 25, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama mitambo ya kusindika maziwa na bidhaa zake wakati walipotembelea kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante Ole Gabriel, Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya ASAS na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wa Mkoa wa Iringa, Salim Abri, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na wanne kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Fuad Abri na wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakizungumza na Balozi wa bidhaa za maziwa za ASAS na Msanii maarufu nchini, Mai Zumo wakati walipotemblea kiwanda cha maziwa cha ASAS cha mjini Iringa, Septemba 25, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: