Mvua zinazoendelea kunyesha mkoa wa Tanga zimezidi kuleta maafa, baada ya usiku wa kuamkia leo Oktoba 26, 2019 kukata barabara kati ya Handeni na Korogwe katikati ya kijiji cha Misima na Sindeni. Pichani ni gari la abiria aina ya Noah likiwa limetumbukia mtoni. Noah hiyo inayodaiwa ni ya abiria, na ilikuwa inatoka Handeni kwenda Korogwe, ilipofika hapo alfajiri ya leo, dereva hakujua kuwa barabara imekatika, hivyo akajikuta anaingia kwenye mto. Inadaiwa watu kadhaa wamepoteza maisha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: