Mkurugenzi Manispaa ya Singida Bw. Bravo Kizito ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa klabu ya Wafanyabiashara wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Mkoani Singida ambao umehusisha Wafanyabiashara wa wakubwa, wa kati na Wadogo. Uzinduzi uliofanyika jana Oktoba 3, 2019 mjini Singida. Lengo la Klabu hiyo ni kutengeneza mahusiano kati ya mfanyabiashara wadogo na wakubwa kuweza kuboresha biashara zao. Pia kuwaweka karibu na taasisi za kiserikali zinazojiusisha na Mapato (Kodi), Bima, Leseni.
Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wa kati (Head of SME) wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw. Evance Luhimbo akizungumza katika Uzinduzi wa klabu ya Wafanyabiashara wa Benki ya NBC Mkoani Singida uliofanyika mjini humo.

Afisa Biashara Manispaa Singida Bw. Erick Semkwembe akizungumza katika Uzinduzi wa klabu ya Wafanyabiashara wa Benki ya NBC Mkoani Singida uliofanyika mjini humo.
Wafanyabiashara na wageni waalikwa wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika Uzinduzi wa klabu ya Wafanyabiashara wa Benki ya NBC Mkoani Singida uliofanyika mjini humo.
 Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wa kati (Head of SME) wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw. Evance Luhimbo akifuatilia.
Meneja Mahusiano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw. William Kallage akizungumza katika Uzinduzi wa klabu ya Wafanyabiashara wa Benki ya NBC Mkoani Singida uliofanyika mjini humo.

Wageni waalikwa wakicheza na Mkurugenzi Manispaa ya Singida Bw. Bravo Kizito ambaye alikuwa mgeni rasmi (wa pili toka kushoto) mara baada ya kuzindua klabu ya Wafanyabiashara wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Mkoani Singida.
Bw. Mvungi kutoka SIDO mkoani Singida akizungumza machache.
 Wafanyabiashara na wageni waalikwa wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika Uzinduzi wa klabu ya Wafanyabiashara wa Benki ya NBC Mkoani Singida uliofanyika mjini humo.
Ofisa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Singida Bw. Zacharia Gwagilo akizungumza machache.
 Wafanyabiashara na wageni waalikwa wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika Uzinduzi wa klabu ya Wafanyabiashara wa Benki ya NBC Mkoani Singida uliofanyika mjini humo.
Mmoja ya wafanyabishara wa mkoani Singida akiuliza swali mara baada ya kusikiliza mada zilizokuwa zikitolewa katika Uzinduzi wa klabu ya Wafanyabiashara wa Benki ya NBC Mkoani Singida uliofanyika mjini humo.

Na Mwandishi Wetu.

Benki ya Taifa ya Biashara, NBC imezindua klabu ya wafanyabiashara wa mkoani Singida.

Akizungumza katika uzinduzi huo mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wa kati (Head of SME) Bw. Evance  Luhimbo amesema kuwa klabu hiyo ya wafanyabiashara imehusisha wale wakubwa, wakati na wadogo lengo ikiwa ni kutengeneza mahusiano ili kuweza kuboresha bisahara zao.

Ameongeza kuwa klabu hiyo itawaweka karibu wafanyabiashara na taasisi za kiserikali ikiwemo Mamlaka ya Mapato (Kodi), Bima na Brela katika ufuatiliaji wa leseni mbali mbambali wanazohitaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Bravo Kizito amewataka wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Singida waliokuwepo kwenye klabu hiyo kuwa na umoja, upendo na mshikamano.

Alisisitiza kuwa ni vyema wafanyabiashara wakaitumia kwa benki ya NBC kwani kwasasa huduma zao zimeboreshwa na zimekuwa rafiki.

Pia amesisitiza kwa ya Benki ya NBC kuongeza vituo vya kutolea huduma mkoani Singida kwani kwa Sasa vipo (16) ili kuwafikia watu wengi zaidi.

"Nawapongeza kwa kazi nzuri NBC, nawapongeza wafanyabiashara kwa kujiunga kwenye klabu hii, nampongeza Raisi John Pombe Magufuli kwa juhudi zake kwa Benki zetu za Tanzania kwani amekuwa mkombozi wetu hususani kwa wajasiliamali wadogo ili kufikia malengo yao na kuwa wafanyabiashara wakubwa hapo baadae," amesema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: