Kundi la makampuni inayoongoza barani Africa ya Liquid Telecom imemteua bwana Hussein Kitambi kama Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni ya Raha Liquid Telecom Tanzania kuanzia tarehe 1 Oktoba 2019. 

Bwana hussein anakuja na uzoefu wa kimataifa kutoka katika kufanyakazi kwenye sekta ya mawasiliano na vile vile ametumikia katika nchi mbalimbali barani Afrika. Anakuja na rekodi za kuthibitika katika kuboresha utendaji wa uendeshaji, kuongoza biashara katika mabadiliko pamoja na kutekeleza mikakati ya biashara kufikia matokeo halisi ya kiuendeshaji. 

Adil El Youssefi, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Liquid Telecom Kanda ya Afrika Mashariki, amesema: "Tunashauku kubwa katika mambo yajayo ya kampuni ya Raha Liquid na tunaamini kwamba Hussein atafikisha kampuni hii katika hatua ya juu zaidi. Kipaji chake, maono yake na mtazamo wake utajenga mahusiano mapya, kubadilisha biashara na kuleta mabadiliko chanya katika biashara." 

Kabla ya uteuzi huu, Bwana Hussein alikuwa anafanya kazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa SimbaNET akisimamia uendeshaji nchini Kenya, Uganda na Tanzania, ambako alikuwa anahusika na mifumo ya kibiashara kwa makampuni na mifumo ya wafanyabiashara wadogo na wakati. 

Wakati huo huo, Hussein vilevile alikuwa anatumikia kama Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Wananchi Tanzania akisimamia masoko ya biashara kwa biashara (B2B) na biashara kwa Makampuni (B2C) Kabla ya nafasi hii alifanyakazi kama Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Wananchi Business Service Unit (WBC) katika kitengo cha biashara cha kundi la makampuni ya Wananchi lenye makao yake makuu nchini Kenya. 

"Ninatazamia kufanya kazi kwa ukaribu na wateja nchini Tanzania na kuwasaidia kufikia mapinduzi ya kidigitali," alisema Hussein.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: